ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 24, 2013

Watu 60 wanusurika kifo ajali basi la Hajees

Costantine Massa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,
Zaidi ya watu 60 wamenusurika kufa huku wengine wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Hajees lenye namba za usajili T136 BES walilokuwa wakisafiria kutoka Arusha kwenda mjini Tanga kupinduka wilayani Muheza.
Ajali hiyo ilitokea juzi katika kijiji cha Tanganyika wilayani humu wakati basi hilo likitokea Arusha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo chake kilitokana na kupasuka kwa tairi la mbele na hivyo dereva akashindwa kulimudu.

Kamanda Massawe alisema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali Teule Muheza kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
CHANZO: NIPASHE

No comments: