RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.
Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).
Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”
Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”
Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.
“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.
Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.
Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.
Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.
Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.
Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.
7 comments:
Watz tuwe positive,so what akiwa raia wa Rwanda/Tanzania? Ni mwafrica ambaye ni smart,lets utilize our own brains, Mr.Kagame is the smart president,anajali what u can deliver. Tuache hatred/wivu usio na tija. Wataalam kama madaktari tunawafukuza,wameenda Rwanda,wameula,sisi tunabaki kulaumu,aaghh! Inachosha! " Emancipate urself from mental slavery" by Bob Marley.
Ni myarwanda aliekua akihishi TZ. make it clear .Wapo wengi tu waliamia miaka ya 70s to 80s ,na wengine niwajuzi juzi tu
Hivi wewe uloandika comment ya kwanza mbona una jazba namna hiyo au huelewi kilichoandikwa? ivi umeona wapi mtu alokasirika hapo? mpaka uandike hivyo? hayo ni maelezo tu yanayomuhusu huyo muheshimiwa baba yake ni nani amezaliwa wapi na amesomea wapi hakuna alosema kuwa alichoamua ni kibaya, soma habari na uielewe ndio ucomment
hana cha utanzania huyo..sema mnyarwanda aliekulia tanzania na kusomeshwa na pesa za wavuja jasho wa tanzania aula rwanda period!!wako weengi dizaini hio tunao mitaani.
Mkuu, hakuna hapo ameona wivu au hatred, mwandishi wa habari ka post habari tuu ya kusema mheshimiwa alikuwa mtanzania, infact kama umesoma habari vizuri unaweza kuiweka in positive way kwa sababu mwandishi katoa sifa za jamaa sana na kazi nzuri aliyoifanya mpaka akafikia hapo alipo kuwa waziri na hata ndugu zake they are proud of him... may be badala ya kulalamika hatred na sijui vitu gan which doesn't look like kwenye habari hii may be we can discuss jinsi gani watanzania na Taifa letu linaweza kunufaika kwa kupitisha dual citizeship...lawama na accusations hazitatupeleka kokote as watanzania.
Sijaona mwandishi kalalamika au anaona wivu au analia kwa nini jamaa kabadilisha uraia,kasema alikuwa mtanznia kaukana uraia..it may be up to us watanzania kufikiria kubadilisha system ya nchi yetu!!!!!!!
Tatizo la kutokuwa na uraia wa nchi mbili. Ingekuwa tuna sheria ya uraia wa nchi mbili, huyu prof angeendelea kuwa raia wa TZ na TZ ingenufaika kwa njia moja au nyingine kiuchumi (mzunguuko wa kifedha).
Mdau wa kwanza uko on point,why mention uraia na sio mema aliyofanya. Then change the title. Jibu hoja,kuna umuhimu gani kujadili uzawa/kabila/utaifa etc. Tujadili Mtz aliyepata nafasi ya juu kwa nchi ya kigeni. Wako wengi tu wenye vyeo nje ya nchi . Wanaitangaza vyema bongo yetu. For all of them,kudos to you all.!!! Keep up the good work
Post a Comment