Friday, February 22, 2013

MATOKEO YA KIDATU CHA 4 NI JANGA KWA TAIFA

2008-2012: Div 4 and Zero

Chart ya Matokeo ya Form IV, 2002-2012


Wakati Dk Ndalichako Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania, NECTA, (pichani) akielezea yaliyojiri kwenye karatasi za majibu ya mitihani ya kidato cha nne mwaka huu (ikiwemo kuonyesha madudu ya kijana wa kitanzania aliyechora "Zombi" kama picha inavyojionyesha) mdau mmoja wa Diaspora (hapa tutamuita "Chinga" wa Kijiwe cha South) alitumia dakika chache wakati akisubiri mlo wake wa mchana "akigoogle" press conferences za Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Kama itakavyosomeka kwenye chart mbili za 2008-2012 ;moja ikionyesha Div IV and O, nyingine Div I, II, III & IV (iliyotayarishwa na mwanaKJW mwingine zinavyoonyesha) asilimia ya wanafunzi wanaopata Div 1-3, imekuwa ikiporomoka mno tangu 2008. Pamoja na kwamba Division 4 nayo imekuwa ikiporomoka, vielelezi vinaonyesha Daraja 0 limekuwa likiongezeka kwa kasi ya ajabu. Mtazamo wa haraka unaonyesha kwamba namba ya wanafunzi wanaojiandikisha kwa mitihani ya Kidato cha Nne (Form IV)exam haijaongezeka, at least not dramatic, hivyo uchambuzi wa haraka utaonyesha kwamba kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi Division 4 unaweza ainishwa na ongezeko la wanafunzi wanaoporomoka zaidi kutoka Div 4 kwenda Div 0! (We know they are NOT going to Div 1,2,or 3).

This is just a quick snapshot. Waandishi wengi wa habari wana show up kwenye press conference kichwa chini, macho kwenye note books na akili makini kunukuu neno kwa neno, which ni moja ya changamoto (kunukuu kwa usahahi yanayotamkwa). Wapo wengine wenye tape recorders. Changamoto: inafahimika changamoto ya waandishi wa habari ni nyingi, ndio maana tuna uhaba wa waandishi wenye calibre ya mfano wa Stan Katabalo (R.I.P), James Nhende (also R.I.P), Jenerali Ulimwengu (we can't depend on him alone) etc etc.

Kama ikibidi waandishi wanukuu mdahalo kutoka "Vijimambo", basi natoa changamoto tuwasaidie kuanalyse; "Matokeo mabaya ya Form IV, JE TUFANYE NINI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU?


1 comment:

Anonymous said...

Hivi inawezekana hawa watoto wakapigwa msasa, then wa reseat pepa in 90 Days or so?....these are too many kidz to be dropped off like this jamani!