ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 15, 2013

JK aongoza mazishi ya Askofu Msarikie

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi . Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

Rais Jakaya Kikwete, jana aliongoza maelfu ya waumini, maaskofu, watawa na viongozi wengine wa dini na serikali wa ndani na nje ya nchi katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi kwa zaidi ya miaka 20, Amedeus Msarikie (82).

Katika mazishi hayo yaliyofanyika ndani ya kanisa la Kirsto Mfalme mjini Moshi, na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Papa ambaye alitoa salamu kutoka kwa kiongozi wa kanisa hilo duniani, maaskofu wa majimbo mbalimbali, mawaziri, viongozi wa kisiasa, yalitanguliwa na ibada ya mazishi iliyoanza saa 4:00 asubuhi.


Akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya serikali, Rais Kikwete alisema Msarikie alikuwa kiongozi hodari kwenye kulisimamia kanisa na maendeleo ya kijamii, yaliyonufaisha waumini wa kanisa hilo na wa dini nyingine.

Alisema alisimamia kidete kuhakikisha elimu inakuwa kuanzia ngazi ya awali hadi Chuo Kikuu, na kuwa mhasisi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Mwenge (MUCE), ambacho kinatoa walimu wa masomo ya Sayansi.

“Mwenge ni Chuo Kikuu ambacho kinalipatia taifa walimu wa masomo ya Sayansi ambao wanahitajika sana kwenye shule zetu, tutamkumbuka na kumuenzi kwa mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake kwa wanadamu wenzake kwa manufaa ya Taifa letu,” alisema Rais Kikwete.

Aidha, aliwataka viongozi wa kanisa hilo na waumini kumuenzi kwa kuendelea kutumikia kwa uaminifu, kiongozi mwema aliyehubiri upendo,amani, mshikamano na upendo na kujiepusha kufanya vitendo kinyume na alivyosimamia.

Salamu kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), zilimemuelezea Askofu Msarikie kuwa alikuwa mshiriki mzuri wa maendeleo ya kanisa na jamii na alikuwa mwenyekiti wa Idara ya Uchungaji tangu mwaka 1987 hadi 2007 alipostaafu Uaskofu.

Akiwasilisha salamu kwa niaba ya dini nyingine, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu
Dk. Martin Shao, alisema kanisa limepoteza kiongozi mahiri katika masuala ya kiroho na kijamii na kwamba ni wajibu wa waumini na viongozi kuiga mema yote aliyoyatenda wakati wa uhai wake.

Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa; Waziri wa Nchi ofisi ya
Rais (Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira, wabunge; wakuu wa mikoa ya jirani, wakuu wa wilaya, na viongozi wa vyama vya siasa na taasisi.

No comments: