Blog ya
Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico na Jumuiya ya
Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea
miaka 3 ya Vijimambo kwa kuendeleza Lugha na Utamaduni wa Kiswahili. Madhumuni
ya hili tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ya
Kaskazini ili watoto wanaoishi huku Marekani ya Kaskazini waweze kuendeleza
matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi.
July 6, 2013 hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo
207 w Hampton Pl,
Capitol Height, MD
Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekaniyote ni kudumisha utamaduni wa kiswahili Marekani ya Kaskazini
TEGA SIKIO HABARI ZAIDI ZITAFUATA
-------------------------------------------------------
kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165 Asante
No comments:
Post a Comment