Wednesday, February 27, 2013

TAARIFA KUHUSU VITUO VIWILI VYA RADIO KUFUNGIWA TANZANIA.

Serikali ya Tanzania kupitia kamati ya maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia kwa muda wa miezi sita vituo vya radio ya Iman Morogoro na radio Kwa Neema Mwanza kutokana na kukiuka kanuni na taratibu za utangazaji kinyume na sheria namba 5 ya utangazaji ya mwaka 1993.
Makamu mwenyekiti wa hiyo kamati Walter Bigonya amesema kwa time tofauti hivyo vituo vimekua vikishiriki kurusha matangazo ya uchochezi kwa Watanzania ambapo Iman wamedaiwa kushiriki kuhamasisha watu wasishiriki zoezi la sensa ya watu na makazi wakati kituo cha redio cha kwa Neema kimeshiriki kueneza uchochezi juu ya kuchinja kati ya Waislamu na Wakristo.
Kwenye hatua nyingine kamati hiyo imekipiga faini ya shilingi milioni 5 kituo cha radio cha Clouds Fm kutokana na kurusha matangazo yanayoashiria uhamasishaji wa vitendo vya kishoga kupitia Power Breakfast january 23 2013 ambapo Mkurugenzi wa utafiti na uzalishaji Ruge Mutahaba amesema uongozi umepanga kukata rufaa kupinga hiyo adhabu ili kutoa nafasi zaidi ya kufanyika uchunguzi wa hayo madai.

No comments: