January Makamba.
Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines za AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kupata comments nyingi ni stori ya kauli ya Naibu Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Mh. January Makamba.
Ni kuhusu ishu ambayo imepita kwenye midomo ya watu wengi ya mpango wa Uongozi wa Bunge kutoruhusu tena bunge liwe linaonekana LIVE kwenye TV.
Maoni ya Mh Makamba ni haya…. “sikubaliani kabisa kwamba bunge lisitangazwe, bunge ni chombo cha wawakilishi wa watu lazima watu wapate fursa ya kuwaona watu waliowachagua wanafanya kazi gani, ni vizuri likawa linatangazwa moja kwa moja bila kuhaririwa sehemu yoyote”
Kwenye sentensi ya pili Mh. Mkamba anasema “Pamoja na kwamba kuna vituko bungeni lakini ni vyema wananchi wakaona watu waliowachagua wanafanya vituko gani vilevile itawasaidia kuamua wakati watachagua tena, kuna faida wala hakua hasara yoyote kwa bunge kuonyeshwa moja kwa moja, niliombwa nitoe maelezo kwa wabunge kuhusu kuhama kutoka kwenye mfumo wa analog kwenda digital na changamoto zilizopo na kwa nini tumehama, wakati nazungumza nikatoa ushauri kwamba moja ya faida za mfumo huu mpya… sasa hivi inawezekana kabisa mtu au watu au taasisi ikawa na channel yake ya TV”
Naibu Waziri January Makamba ambae pia ni mbunge wa Bumbuli kwenye sentensi ya kumalizia amesema ” hauhitaji kituo cha Tv ili urushe matangazo yako, nikasema Bunge kwa mfano badala ya kutangazwa kupitia TBC linaweza likawa na channel yake kwenye king’amuzi ambayo inatangaza bunge moja kwa moja na saa zote na kunakuwa na marudio jioni ya kile kipindi cha asubuhi na channel hii inatangaza bunge saa 24, sio bunge tu hata kazi za kamati… mimi ni muumini mkubwa wa uwazi na ningependa kabisa kwamba bunge litangazwe wakati wote liwe Live”
No comments:
Post a Comment