Tuesday, February 5, 2013

WANANCHI IRINGA WALISHWA MZOGA ,MUUZAJI ATIMUA MBIO

Vijana wakionyesha kaburi ambalo mzoga huo wa ng'ombe ulizikwa likiwa na mabaki ya nyama
Haya ni mabaki ya mzoga huu baada ya kuzikwa tena leo
TABIA ya baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa kupenda nyama nyama bila kuangalia ni wapi wanakula ama kununua nyama hiyo ,imewatokea puani wakazi wa Ikonongo kata ya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa baada ya kuuziwa nyama ya mzoga wa ng'ombe aliyekufa kwa sumu toka usiku wa jana.

Wananchi hao wamejikuta katika majuto baada ya kujisikia dalilia za matumbo kuuna baada ya kufakamia nyama hiyo ya mzoga kwa zaidi ya siku mbili sasa.

wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo baadhi ya wafanyakazi wa shamba la mifugo la raia wa nchini China ambao walishuhudia kifo cha ng'ombe huyo na kuzikwa kwake ,walisema kuwa ng'ombe huyo alikufa toka jana na kuzikwa baada ya kuchukuliwa vipimo na kuonekana kifo chake kimesababishwa na sumu .

Bila kutaja aina ya sumu iliyopelekea kifo cha ng'ombe huyo walidai kuwa baada ya kupimwa lilichimbwa shimo kubwa na kufukia mzoga huyo huku mwenzao huyo akionyesha tamaa kwa kuwaomba wasifukie sana mzoga huyo.

Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la kufukia mzoga huyo inadaiwa kuwa mwenzao mmoja aliyefahamika kwa jina la Abdu alirudi usiku na kufukua mzoga huyo na kumchunja ngozi kisha kupeleka kijiji kufungua bucha la nyama na wananchi wa eneo hilo kuchangmkia kununua nyama hiyo ya bei ya kutupwa .

Salome kalinga ni mmoja kati ya wakazi wa Ikonongo ambae alipata kula nyama hiyo amesema kuwa bei ya kutupwa ambayo nyama hiyo ilikuwa ikiuzwa ndio iliwasukuma wananchi wengi kuchangamkia nyama hiyo na hata kununua ya kutosha kwa kwenda kuweka akiba majumbani kwao.

"Sisi tuliambiwa kuwa mchina huyo ameamua kutoa sadaka kwa wakazi hao kwa kumkubali kuwa muwekezaji katika eneo hilo hivyo kilo la nyama badala ya kuuzwa shilingi 5000 kama ilivyo buchani kijana huyo alikuwa akiuza shilingi 2000 hadi 1000 na iwapo unapungufu unaongea"

Alisema kuwa baada ya kula nyama hiyo kwa siku mbili mfululizo sasa ndipo leo wamebaini kuwa nyama hiyo si nyama tena bali ni mzoga na hivyo kuamua kufanya msako na kufanikiwa kuwakamata wauzaji wawili akiwemo kijana huyo ambae baadae alitoweka.

Hivyo hadi sasa kijana mmoja amekamatwa akiwa na nyama kilo 10 ambazo alikuwa akiendelea kuuza na kupewa kichapo kabla ya kupelekwa polisi.

Tabia ya wananchi wa Iringa kuchangamkia mishkaki na nyama ambayo inauzwa kwa bei ya kutupwa imeendelea kukua na hivyo ili kuepuka kulishwa mizoga ni vema tahadhari zaidi kuchukuliwa na walaji nyama.

Na Francis Godwin wa Iringa Yetu

No comments: