Kutoka kushoto Mussa Linga, George Mwasalwiba, Seif ndossa, Michael Gregory na Edward Taji walipokutwa na kamera ya Vijimambo kwenye Kijiji cha Swahili Jana wakipata Dinner ya mchana kabla ya mchezo wa pili wa robo fainali.
Timu ya Pool yenye maskani yake DMV Jana Jumamosi March 9, 2013 walifuzu hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga wapizani wao kutoka Virginia kwenye mashindano ya Pool yanayoendelea Laurel, Maryland nchini Marekani.
Kocha mchezaji Edward Taji aliiambia Vijimambo kwa njia ya simu, mechi ilikua ngumu lakini nawashukuru vijana wake kwa kucheza kwa ustadi na hatimae kuwezesha ushindi na kuiingiza timu nusu fainali itakayochezewa hapo hapo Laurel sehemu inayoitwa Bank Shorts Bar & Grill. Mechi itaanza saa 10 jioni (4:00 pm) na tunaomba mashabiki wajetupa sapoti. na mshindi wa mashindano haya hupelekwa Las Vegas kwenye mashindano ya mabigwa wa majimbo.
No comments:
Post a Comment