Ndivyo maisha yalivyo, kila mmoja ana kumbukumbu mbaya katika maisha yake ambazo kwa hakika hapendi kuzikumbuka mara kwa mara. Kuna mambo yanayoumiza ambayo kwa kawaida binadamu wengi hawapendi kukumbuka machungu.
Ndiyo maana binadamu mwenye utashi huyaacha yaliyopita yabaki nyuma na kusonga mbele, mambo ya nyuma yanabaki kuwa somo au daraja la kumfikisha kwenye eneo lingine. Hayo ndiyo maisha.
Marafiki zangu, nimeamua kueleza yote hayo kama utangulizi ili iwe rahisi kuzungumzia mada hii. Katika mapenzi, wengi hukutana na wenzi wao ukubwani (nikimaanisha kuanzia miaka 18 na kuendelea).
Maisha ya nyuma ya mwenzako si rahisi kuyajua kwa undani. Unaweza kuchunguza baadhi ya mambo kwa lengo la kukusaidia kumjua mwenzako vizuri au kwa bahati mbaya au nzuri akatokea mtu na kukuanikia maisha ya nyuma ya mwenzako. Kwenye tatizo ni pale ambapo utaelezwa mambo ambayo hutayafurahia.
Utaelezwa maisha yake mabaya, uhuni na tabia za hovyo alizowahi kufanya mpenzi wako. Unaweza kumchunguza msichana wako, ukakutana na mtu akakumbia: “Daah! Yule demu hafai kabisa, mtaa mzima huu kauchafua, ameshatembea hadi na wazee.”
Utaelezwa maisha yake mabaya, uhuni na tabia za hovyo alizowahi kufanya mpenzi wako. Unaweza kumchunguza msichana wako, ukakutana na mtu akakumbia: “Daah! Yule demu hafai kabisa, mtaa mzima huu kauchafua, ameshatembea hadi na wazee.”
Je, kwa hali hii unapaswa kufanya nini? Tabia mbaya za wenzako za nyuma zinaweza kuharibu mapenzi yenu na kuamua kuachana moja kwa moja? Mathalani unaweza kupewa maelezo kwamba, mwenzako aliwahi kutoa mimba huko nyuma na mengine mengi ambayo kwa kawaida hukuyajua au hayapendizi tu!
Marafiki zangu, mada hii imezaliwa kutoka kwa msomaji mmoja aliyeuliza kuhusu mpenzi wake. Alisema: “Kaka Shaluwa, mpenzi wangu nimeambiwa ana tabia mbaya sana. Amewahi kutembea na wasichana watatu ndugu wa familia moja kwa nyakati tofauti. Nasikia alikuwa mlevi sana na watu wote mtaa mzima wanamjua kwa tabia zake mbaya. Naogopa kuolewa naye kutokana na tabia hizo, natamani kumuacha tu. Naomba ushauri wako.”
Nilizungumza naye na kumshauri cha kufanya. Lakini niliona inawezekana wapo wengi wanaokabiliana na jambo kama hili. Wapo wengi ambao wanababaishwa na jambo hili lakini ukweli ni upi?
HISTORIA GANI HASA?
Kimsingi kuna tabia au mambo ambayo hayapendezi kwenye jamii. Kwa kawaida wengi hawapendi kujihusisha na watu wenye tabia au sifa mbaya kwenye jamii.
Nimeshafafanua katika kipengele kilichopita hapo juu lakini lengo hasa hapa ni juu ya miendeno mibovu ya kiuhusiano na wenzi waliopita. Katika hili yapo mambo ya msingi zaidi kuangaliwa kuliko historia ya nyuma. Twende tukaone.
MWANGALIE KWA UPYA
Ukweli uko wazi marafiki zangu, ikiwa hukufahamu tabia zake mpaka ulivyosikia ni wazi kuwa ni mambo ambayo alikuwa akiyafanya huko nyuma. Jambo kubwa kwako kwa sasa ni kumwangalia kwa upya.
Chukua uliyoelezwa, yafanyie kazi kwa kuangalia kama bado ana tabia kama hizo. Rafiki zangu, kukosea nyuma hakumaanishi kwamba ataendelea kuwa yuleyule siku zote. Mwangalie kwa upya alivyo leo.
Wiki ijayo tutaendelea na mada hii, USIKOSE!
GPL
1 comment:
kakwambia nani bwana historia yake tuache, mtu kama alikuwa mbakaji na mpenda ngono skati hapiti kila akionachoa anakitaka wee halafu aje akuambiye ameacha kuwa macho kweli pendo la kweli kila mtu analitaka lakini historia ya mtu pia isikutishe sana lakin pia isikufanye umelala ukasahau wakati mambo hayaendi sawa unafikiria historia yake na kujumlisha na utajaza kama utatoa uachane naye au ubaki kubana naye na kugawanya.
maisha ya siku hizi bwana kila mtu anahitaji kuwa muaminifu na kujihadhari hakuna mapenzi ya kweli na ukiingia kwenye relationshipi jiulize unataka nini utapata nini thats it, na je anakuridhisha uko tayari kuishi na kufa naye mpaka uzeeni au vipi.
akili kichwani hakuna mapenzi ya kweli japo kuwa kila mtu tunayataka kwa sababu wote tuna tamaa zetu katika maisha lakini ukimuweka mungu mbele katika kila kitu chako ukifanyacho na kumuamini yeye basi nakuhakikishia utapata pendo la kweli na la dhati na lakudumu daimia na mwenzio pia awe mcha mungu sio wewe mcha mungu mwenzako mfuta bangi na wa kichochorini baaabaa kila kona
kazi kweni..
mropoka ovyoo wa NY LAKINI MSEMA KWELI UKIYACHUNGUZA MANENO YANGU
Post a Comment