Na Dustan Shekidele, Morogoro
FAMILIA ya mlemavu, Msafiri Jeremia mkazi wa Kijiji cha Munisagale,Kilosa mkoani hapa imetoa shukrani kwa Kampuni ya Global Publishers iliyoandika habari kuhusu mateso yanayomkabili na kufanikiwa kupewa msaada wa shilingi 571,145 na wasamaria wema.Mlemavu huyo mwenye mke na watoto watatu, akizungumza na mwandishi wetu (pichani kulia) aliyefika nyumbani kwake kumkabidhi kiasi hicho cha fedha, alisema anaishukuru Global kwani bila kuandika habari hiyo asingesaidiwa.
“Kwa kweli nashindwa namna ya kushukuru kwa msaada nilioupata kutoka kwa wasamaria wema baada ya habari zangu kuandikwa kwenye Gazeti la Uwazi, Mungu awabariki sana,” alisema Jeremia.
Aidha, mkazi mmoja wa Tabora amemchukua mtoto mkubwa wa mlemavu huyo aitwaye Saimon kwa lengo la kumpatia ajira kwenye kampuni yake, pia dada mmoja alimchukua binti yake Magreth na kumpa ajira kwenye saluni anayoimiliki.

Habari kuhusu mlemavu huyo aliyekatika mkono na mguu katika ajali ya treni iliyotokea Msagali, Dodoma mwaka 2000.
GPL
No comments:
Post a Comment