Lakini kumekuwa na malalamiko ya upande mmoja kumlaumu mwenzake kuwa hamtoshelezi sana, au mwingine anaonekana kujifikiria zaidi yeyey kuliko mwenzake. Hilo ni tatiozo kubwa sana kwa wapenzi.
Inawezekana kabisa wewe upo katika uhusiano na mpenzi wako kwa muda mrefu sana, lakini hata siku moja hujawahi kufurahia mapenzi. Pia si ajabu kwamba, hujawahi kufika kileleni tangu siku ulionza kuwa katika uhusiano na mpenzi wako.
Lakini pia, upo mjadala kwamba, ni nani kati ya mwanamke na mwanaume huwa haridhiki zaidi kimapenzi kuliko mwenzake? Huu ni mjadala mpana, lakini wenye dawa.
Kwa heshima kubwa, naomba kuuwasilisha kwenu, nikitaka maoni yenu, ukieleza kwa ujuavyo wewe kati ya mwanaume au mwanamke ni nani anawahi kufika mshindo na kumuacha mwenzake bado ana kiu?
Je, wewe ni jinsia gani? Unaridhishwa na mapenzi ya mpenzi wako? Kama ndivyo kivipi? Kama siyo, kwanini? Si vibaya pia kama utaeleza nini kifanyike, ili wapenzi wanapokuwa faragha, wapate usawa.
Baada ya maoni yenu, nitakuja na dawa ya kitaalamu kabisa. Haya sasa wadau kazi kwenu kuchangia.
Shaluwa
No comments:
Post a Comment