Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile
Watu watatu wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti akiwemo mama aliyeuawa na mwanaye na watoto wawili kuliwa na mamba.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema katika tukio lililotokea Machi 14, mwaka huu, majira ya jioni huko Chamwino Manispaa ya Morogoro, mwanamke mmoja Dorcas Lugano (55) aliuawa kwa kupigwa shoka ubavuni baada ya kumtaka mwanaye akatafute kazi ili aanze kujitegemea baada ya umri kuwa mkubwa.
Awali mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kushuhudia umati mkubwa wa watu waliofika eneo hilo kushuhudia mauaji hayo, ambapo baadhi ya waliohojiwa walidai kabla ya tukio hilo, kuliibuka ugomvi baina ya mwanamke huyo na mwanaye, Frank Hilari, ambapo mama huyo alitoka mbio na kukimbilia nyumba ya jirani.
Hata hivyo mashuhuda hao ambao walikataa majina yao kutajwa, walidai baada ya hali hiyo, mtoto huyo, alimfuata nyuma mama yake na kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa na mwanamke mmoja mzee, ambaye alishindwa kuamulia na kumpiga shoka mama yake, na kusababisha kifo chake.
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya watu walimdhibiti asiendelee na madhara kwa watu wengine waliokuwa jirani, kwa kumfungia ndani hadi pale polisi walipofika na kumchukua kumpeleka kituo cha polisi.
Kamanda Shilogile, alikiri kuwa mtuhumiwa amekamatwa na polisi na inasadikiwa kuwa kijana huyo ana matatizo ya akili lakini uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani.
Akizungumzia matukio mengine, Kamanda huyo wa Polisi alisema Machi 13, mwaka huu, majira ya saa 10 jioni huko Vigolegole kata ya Bwakila wilaya ya Morogoro, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mngazi Cosmas Bernad ( 8) alikutwa amefariki dunia baada ya kuliwa na mamba.
Alisema kuwa mtoto huyo alichukuliwa na mamba siku tatu kabla ya kifo chake, wakati akinawa katika maji ya moto Mgeta hadi Machi 13 mabaki ya mwili wake yalipoonekana katika mto huo.
Wakati huo huo, mtoto mwenye umri wa miaka sita, Sikudhani Juma, aliliwa na mamba wakati akiogelea na wenzake katika Mto Ngerengere na hadi sasa maiti yake haijaweza kupatikana.
Shilogile alisema tukio hilo lilitokea Machi 12, mwaka huu, majira ya saa 11 jioni huko Ngerengere katika wilaya ya Morogoro.
Aidha Ibrahim Jaribu mkazi wa eneo la Sia Ujenzi katika kata ya kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwachoma moto midomo watoto wake wawili Malik Jaribu(5) na Ibarahim Jaribu (10) wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Msavu B baada ya kula karanga zake za biashara.
Imedaiwa baba huyo aliwachoma moto midomo watoto hao Machi 13, mwaka huu saa 9.45 jioni baada ya watoto hao kushinda na njaa siku nzima na kuamua kula karanga hizo.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment