ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 20, 2013

MTAZAMO WANGU JUU YA ARTICLE YA NINI HATIMA YA JUMUIYA NA VYAMA VINGI


Article ni nzuri na imejikita kwenye kuhakikisha DMV tunakua na umoja na mshikamano. Safi sana na nimeipenda kwa hilo. Baada ya kuisoma na kuitafakari kwa undani nimegundua  inamapungufu kidogo kulingana na mtazamo wangu BINAFSI. Kwanza, inaonekana inapendekeza kuwa mtu akiwa mwanachama wa chama cha siasa asiwe mwanajumuiya. Hili ni kosa, kwani mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote na akawa mwanajumuiya. Ni dunia huru na watu wanauhuru wa kupenda watakalo. Kinacho takiwa ni  kutofautisha itikadi za vyama na jumuiya.

Pili, nakukoti "ndugu zangu mlio ingia na huyu shetani ondoeni huu uchuro na TUACHENI na umoja wetu". Kwa hili inaonyesha dhambi ya ubaguzi unayo au inakunyemelea. Nadhani cha msingi ungesisitiza watu wawe na vyama vyao lakini wasichanganye na jumuiya. Ni mbaya kutaka kumtenga mTanzania kwa kuwa yupo CCM, CUF au CHADEMA. Ni sawa na kumtenga muislam au mkrito- au kuleta ukabila. Siamini kamanda umetoa kauli hii. Hawa watu wote wana haki ya kupenda chochote na wana hisia kama ulizo nazo wewe za kuamua kupenda jumuiya tu. Ni dunia huru na wana haki ya kufuata watakalo. Ungesisitizia wajitahidi kutofautisha itikadi za jumuiya na vyama vyao vya siasa na sio kuwashinikiza waache vyama vyao na wajiunge na jumuiya la sivyo, « TUACHIENI JUMUIYA YETU ». Kwa kauli hii, wanaweza kukuachia jumuiya yenu.

Tatu, umetoa mfano wa uchaguzi wa chama flani juzi na inaonekana unachuki na watu flani kwenye hicho chama. Kwa maelezo yako haya kuwa « mkitambulishwa huku mkiinua pua » « pelekeni tamaa zenu huko » »au ondokeni kwenye jumuhiya yetu mara moja ». Haya ni maneno yasio ashiria amani na ni ya ubaguzi. Nakushauri ungetumia chaguo la maneno bora zaidi. Haya ni maneno makali na hayawezi kujenga bali kuzidisha chuki. Sishangai umekuja ANONYMOUS. Jitahidi kuja na identity yako muda mwingine ili message iwe na nguvu. Hii itaonyesha unaongea unacho simamia. Talk the talk, walk the walk.


Nne, umeonglea kuwa, miaka minne iliyo pita umekuwa ukikutana na watu kweye jumuhiya na matukio ya kiTanzania wanakuuliza wewe ni chama gani na kama unataka kadi. Nadhani hii ni kwa watu wale wanao kuwa wamepata uongozi na hawana sifa ya kuongoza. Moja ya sifa ya kiongozi ni kuunganisha watu na kuweza kutofautisha kati ya siasa na mambo ya kijamii/jumuhiya. Ni wewe binafsi unaweza kemea hili kama upo kwenye shughuri ya kijamii/jumuhiya na mtu analeta siasa unaweza kemea na tabia ika koma. Kwa kupata jibu la swali lako ulilo uliza, waulize hao wanao taka kuuza itikadi za vyama vyao kwenye sherehe za kijamii.

Swala la kiongozi kutaka kuongoza jumuhiya na chama cha siasa, kwa mtazamo wangu, kama anabusara ya kutenganisha mambo ya itikadi na jumuhiya hakuta kuwa na tatizo. Tatizo litatokea iwapo ataingiza maswala ya itikadi ya chama chake kwenye jumuiya. Pia baba  wa taifa alipo sema waogopeni kama  ukoma, hakuzungumzia watu wanao taka madaraka mawili (Kumbuka : yeye alikuwa mwenyekiti wa chama na Raisi), bali wanao kimbilia ikulu. Refer hotuba yake Mbeya mwanzoni mwa miaka ya 90 nadhani 93.

Mwisho umeongelea swala zuri sana la kudumisha amani na umoja. Inavyo onekana wewe ni kiongozi wa jumuiya au mwanachama hai wa jumuiya ya DMV. Ninge kushauri utumie uanachama wako wa jumuiya kuishinikiza jumuiya kutoa TAMKO na sauti MOJA kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu zinazo tokea nyumbani. Isiwe jumuiya kwa ajili ya kuzikana na sherehe tu. Hili swala si la chama cha siasa. Tunaona mengi yanatokea nyumbani, waandishi kutekwan na kuteswa, watu kupigwa risasi hazarani, mauaji ya mashekhe na mapadri. Kwa kifupi watu wananyang’anywa haki yao ya kimsingi, HAKI YA KUISHI. Natoa challenge kwa jumuiya, tuunganisheni na toeni tamko juu ya ukiukwaji wa haki unao endelea Tanzania. Jumuiya isiwe kwa ajili ya kuzikana na sherehe tu.

Addendum ; Nakili kuwa kumekuwa na mtafauruku kati ya waTanzania waishio DMV tokea mambo ya jumuiya na vyama vya siasa kushika kasi maaeneo haya. Lakini baada ya kufanya uchunguzi kidogo nikakundua sintofahamu hii inasababishwa na watu ambao wanafuata mkumbo na hawajui wanacho taka. Hawa watu hufuata watu au upepo na sio itikadi za vyama. USHAURI ; FUATA MISINGI NA KANUNI ZA CHAMA NA SIO WATU.


Liberatus Mwangombe

Twitter @bagasa80

DMV.

15 comments:

Anonymous said...

Big up libe kumbe saingine una akili

Anonymous said...

Asante sana Bwana Libe! wafuata mkumbo, wasiosoma fine prints na kutosimamia mistari ndio hao wayumbao. Kila chama kina itikadi yake. Juwa undani wa habari ikiwa ni pamoja na Historia ndio ujenge hoja. Inaonyesha kuwa tunahitaji madarasa ya kurefresh Elimu na fahamu zetu!

Mwanajumuiya Mkereketwa DMV

Anonymous said...

So Libe naona hasira zimekupanda sana...haya mambo ya vyama mimi sina mpango nayo hata kidogo. Kwanza huyo aliandika mada hiyo nampongeza sana, anaonekana shule ameingia vizuri sana, sababu amepangalia vizuri arguments zake...nadhani kila mtu ana mtazamo wake na ni vizuri kuwa na arguments kama hizi hili watu wajifunze, napenda kumpongeza mtoa mada wa kwanza juu ya Jumuiya na vyama, nadhani Libe umejibu kwa hasira sana.
Mdau
Texas

Anonymous said...

Safi sana mdogo wangu Liberatus. based on my literature review, article yako imegawanyika katika sehemu kubwa mbili. Sehemu ya kwanza ni maoni yako. No one can go wrong with his/her personal opinion. Sehemu ya pili ni theory. Jumuiya ya watanzania DMV kama independent variable na mauaji Tanzania kama dependent variable. Sifahamu hivi vitu viwili vina uhusiano gani. natambua kabisa kuwa umesoma na utakubaliana na mimi kuwa ili theory iwe relevant ni lazima iwe scientific; ambayo ina meet vigezo hivi 2. Logical consistency 2. Scope 3. Parsimony 4. Testability na 5. Emperical validity. Libe, unaelewa kabisa kuwa theory yako hai-meet those criteria kwa sababu jumuiya ya watanzania DMV inaongozwa na katiba yake iliyoundwa na wana-DMV. Jumuiya hii siyo chombo cha dola cha kukemea mauaji Tanzania. Tanzania kuna serikali na criminal justice system ambayo pamoja na mambo mengine, kazi yake ni kuhakukisha haki inatendeka na kila mtu anayo haki ya kuishi. Pamoja na kumkemea mtoa mada yule wa kwanza kuwa ametumia hasira kushambulia vyama vya siasa inawezekana upo sahihi kuwa lugha au maneno aliyo tumia ni makali kidogo, lakini sioni logic ya wewe kuitupia lawama jumuiya ya watanzanian DMV kwa kushindwa kukemea mauaji Tanzania? Naomba utembelee website ya jumuiya ya watanzania DMV ili usome katiba yake. Nina uhakika kuwa jumuiya mbalimbali za watanzania ughaibuni zina-exercese 'political neutrality' na pia siyo vyombo vya dola. Nakushukuru wewe binafsi na yule aliyeanzisha mjadala huu kwa kutuelimisha. Napenda mjadala huu uendelee kwa kupingana bila kutukanana.

baraka daudi said...

Kaka Libe nakupongeza sana kwa mada yako,kwa kweli ndugu Libe amefungua mjadala mzuri.Sisi kama Watanzania tuna wajibu na nchi yetu,kwanza ni Utanzania halafu itikadi zingine,tunaishi katika nyakati tofauti na hakuna ubaya Mtanzania kuwa mwanachama wa chama fulani au jumuiya fulani. Kaka Libe asante kwa mada,nafikiri ingekuwa ni vizuri tuchangie mada kwa kufanyia utafiti sio ushabiki.

Anonymous said...

Wadau naomba kuuliza; Tanzania kuna matawi ya vyama vya siasa vya USA, UK, CHINA au nchi nyingine yeyote?

Anonymous said...

Mimi simpendi libe.Pale alipokuwa anatukana matusi ya kuwachafua wenzake na kufunguwa group za matusi lakini hili kalielezea vizuri ushauri awaombe msamaha alichemka

Anonymous said...

Naamini mwandishi wa article ya kwanza aliandika kwa nia nzuri, lakini proposal yake ilikuwa misguided kwa sababu inakinzana na civil rights. Watu huru wana haki ya kujiunga na vyama vyovyote, viwe vya kisiasa, michezo, kidini, n.k. Kama proposal kama hiyo ingekubalika, next time atasema hakuna haja ya watanzania waishio ughaibuni kuwa wanachama wa yanga au simba AU kuwa wanachama wa vyama vyovyote vingine other than political parties.

bagasa said...

Anonymous wa March 20, 2013 at 3:54 pm. Kuto kunipenda au kunipenda ni chaguo lako kulingana na information uliyo nayo juu yangu. Yote unayo ambiwa kuhusu mimi hayana REAL IMAGE yangu. Ni perception na mawazo ya watu juu yangu. Umenihukumu bila kujua ukweli.

Labda niweke sawa hili wazi, sijawahi kufungua group la kutukana mtu, nasiwezi fanya hivyo. Ni watu mmeamua kuamini mnacho taka na kueneza sumu ya chuki. Hii ni mbaya kumhukumu mtu b'se of " hear say". Kama mtu atataka discussion kwa hili, nipo wazi. Wasiliana na DJ Lucas atuonganishe au wasiliana nami hapa twittwer @bagsa80

Ni wakati wakuweka naswa, kujua ukweli. Mwenye majungu, fitina na chuki ataendelea kuonge kwenye mgongo wango.

Mwisho, siwezi kukubadirisha kufikiria jinsi unavyo taka kunifikiria. Ni mawazo na mtazamo wako lakini havipresent the real image of LIBE.

Thank you for the infor.

LIE IS ELEVATOR, TRUTH IS STAIRS. YOU'LL SOON KNOW THE TRUTH

Anonymous said...

This is no rocket science! Freedom of association, worship, etc. is central to civil rights. The author of the first article should have centered his or her argument on the need to keep political party activities separate from activities of nonpolitical associations of Tanzanians. Kama shughuli za kisiasa hazifai, basi hazifai popote pale, ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.

Anonymous said...

NIMEPENDA SANA MJADALA HUU KWA SABABU KUBWA MBILI:
1. HAKUNA ANYETUKANA
2. HAKUNA ANAYETUKANWA.
NINAFURAHI SANA KUONA WATU WANA TOFAUTIANA KWA KU-REASON TU, NA SIYO KUVUNJIANA HESHIMA.

Anonymous said...

Ninyi wadogo zangu Liberatus na anonymous wa March 20, 2013 @ 3:45pm nawaomba tukutane pale Kilimanjaro Restaurant kwa mtanzania mwenzetu muda mtakaopendekeza ili tushiriki meza moja na tusaidiane kuondoa hako katofauti kati yenu. Nitalipia dinner na vinyweka. Contact zangu ntampa Mr DJ Luka. Mimi nawapenda sana nyie watoto.

Anonymous said...

LIBe LiBe,

Naona unatokota, kwani mbona wewe ndie uliekuwa ukiongoza kuwachoma moto Viongozi wa Jumuiya ya DMV kwenye Facebook, ka. Vyama Ni Vibaya nje ya Nchi. Kwanini Vyama.

Au unasema vitasaidia kuwazika watanzania nje?.

Au unaseema vitasaidia kuwapa kazi na kuwatafutia kazi?.

Wasomi wangapi walipita na kuitwa na serikali ya Tanzania bila kupitia vyamavya Siasa?.

Au ni wanachama wa CHADEMA, ndio watakuwa wakitembeleana Mahospitalini.

Au wana CCM ndio watakuwa wakiandaa Siku ya Mtaanzania .

Au ni wana CUF ndio watakuwa wakichangishana KUSAFIRISHA miili ya Marehemu.

Unasema Jumuiya ya DMV sio iwe inaangalia sherehe na misiba.

Ulikuwa wapi jumuia ya DMV ilipofanya haya Mwaka Jana na Mwaka huu au Mdomo tu kusahau mema na kuleta Mkorogano?

1. NSSF
2. Maisha Ni Nyumba
3. Azania Bank.
4. Tanzania Day
5. Kuwasaidia watanzania Walio Jela
6. Nafasi za Kazi
7. Free Health Screening Annoucement.
8. Kuwakutanisha Watanzania Kumuaga Balozi- Bureeee.
9. Kuwasaidi watanzania ambao wamekuja hapa hawana sehemu za Kuishi- au ulitaka wakujulishe wewe?- Hili wamelifanya BASI.
10. Kuandaa Hafla ya Kumuaga Mwanamke na Mtaanzania wa Kwanza aliyekuwa Makamu katibu mkuu wa UN.

DARASA LA KISWAHILI WANALIANDA PIA.

Vyama havina Nafasi nje. Kama kuna wanaojiona ni wanasiasa wazuri wapande KLM waende wakajenge nchi Nyumbani.

Anonymous said...

Kwa wale mnaopinga kuwepo kwa shughuli vyama vya kisiasa tumieni nguvu ya hoja siyo hoja ya nguvu. Why against political parties? Why not against sports clubs? Why not against religious groups? Nani kasema huwezi kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa na ukashiriki kikamilifu katika shughuli zisizo za kisiasa kama vile misiba na social events zingine?

Anonymous said...

Nimegundua kuwa watu wanachuki binafsi. Kweli ndugu zangu watanzania mtu unafikia kusema "mimi simpendi Libe" Kisa alikuwa anawatukana watu Facebook. Mnauhakika? Mbona yeye anasema hajafanya hivyo.

Mume muuliza, au ndio mumesikia upande moja wa kesi. Tusipende kuhukumu bila kuwa na uhakika. Ndio maana kuna kuwa na chuki kwa sababu watu hamjui ukweli mnaamini mnacho ambiwa.

Jaribuni kushindana na LIBE wa kupinga hoja zake sio kumpinga yeye binafsi.

Mnatia kichefuchefu