Advertisements

Wednesday, March 27, 2013

Mwili wa mwanafunzi wa UDSM waagwa


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Profesa Yunus Mgaya
Mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Shule ya Sheria mwaka wa pili, Joseph Bernadina (25), aliyefariki juzi baada ya kujinyonga uliagwa jana katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es salaam nakusafirishwa kuelekea Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kwa ajili ya maziko.


Kwa mujibu wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Profesa Yunus Mgaya alisema mwili wa marehemu uliagwa na wanafunzi wa chuo hicho wa shule mbalimbali, Wahadhiri pamoja na wafanyakazi wa chuo na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.

Alisema msafara wa kuelekea Ludewa utasimamiwa na mmoja wa wafanyakazi kutoka ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi ambaye pia atasimamia shughuli nyingine kama mwakilishi wa chuo.

Mwanafunzi huyo alijinyonga juzi kwa kutumia kamba ya manila aliyokuwa ameifunga juu ya mti katika eneo la Yombo, chuoni hapo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: