Papa akiwa katika gari aina ya Mercedes Benz G-Class SUV wakati akipita kwenye viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma.
Mapema, Papa Francis alizunguka katika viunga hivyo akiwa katika gari la wazi, akiteremka kuwabariki mahujaji waliofika hapo.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amewataka viongozi na watu wote duniani kuwalinda wanyonge na watu maskini. Watu wapatao 200,000 wamehudhuria sherehe hizo.
Papa Francis alichaguliwa na mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.
HABARI: BBCSWAHILI, PICHA : AP, REUTERS NA EPA
3 comments:
Naona bendera ya Tanzania ileeeee kwa kushoto.lol.
Wow naona bendera ya Tanzania ileeee.Nice.
Naona bendera ya Tanzania hapo...
Post a Comment