ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 19, 2013

PAPA FRANCIS ATAWAZWA RASMI JIJINI VATICAN LEO

Papa Francis I, akiupungia umati wa watu waliohudhuria sherehe hizo.
Papa Francis akimbusu mtoto wakati akiwasili katika viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro.
Papa akiwa katika gari aina ya Mercedes Benz G-Class SUV wakati akipita kwenye viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma.
Umati mkubwa wa watu waliohudhuria tukio hilo leo.
Rais wa Zimbabwe, Mzee Robert Mugabe pamoja na mkewe Grace nao walikuwepo.

SHEREHE za kumtawaza kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis I, zimefanyika katika viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli zake za Papa.
Mapema, Papa Francis alizunguka katika viunga hivyo akiwa katika gari la wazi, akiteremka kuwabariki mahujaji waliofika hapo.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amewataka viongozi na watu wote duniani kuwalinda wanyonge na watu maskini. Watu wapatao 200,000 wamehudhuria sherehe hizo.
Papa Francis alichaguliwa na mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.

HABARI: BBCSWAHILI, PICHA : AP, REUTERS NA EPA

3 comments:

Anonymous said...

Naona bendera ya Tanzania ileeeee kwa kushoto.lol.

Anonymous said...

Wow naona bendera ya Tanzania ileeee.Nice.

Anonymous said...

Naona bendera ya Tanzania hapo...