Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, namba P 2492 Elikiza Nko, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari mali ya Kanisa la Assemblies of God (TAG).
Aligongwa jana muda mfupi baada ya kutoka kuongoza magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku moja Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 7:00 mchana eneo la Bamaga jijini Dar es Salaam wakati msafara wa Rais Kikwete ukipita ukitokea mjini kuelekea Ubungo.
Kenyela alisema gari lililomgonga ni lenye namba T 328 BML aina ya Landlover Discover na dereva wa gari hilo baada ya tukio hilo alikimbia.
Alisema askari huyo baada ya kuongoza magari ya msafara wa rais alianza kuruhusu magari ya kawaida ndipo gari hilo lilipopita kwa kasi na kumgonga na kufariki papo hapo.
Aliongeza kuwa mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kumsaka dereva na gari aliyesababisha kifo cha askari huyo.
Kamanda Kenyela alitoa pole kwa familia ya askari huyo na askari wa mkoa wa Kinondoni na kutoa onyo kwa madereva kuheshimu taratibu na sheria za barabarani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment