ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 8, 2013

Rais Wa Nigeria Atoa Naira Bilioni 3 Kwa Ajili Ya "PROJECT NOLLYWOOD"...

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametangaza kuanzisha mfuko wa kuwasaidia wasanii wa filamu nchini Nigeria ambao una thamani ya Naira bilioni 3 za kinigeria.
Rais Goodluck ameanzisha mfuko huo na kuupa jina la ''Project Nollywood''ambao ameutolea kiaisi hicho cha pesa kwa ajili ya kufanya kazi za wasanii wa nchini humo kuwa bora na katika kiwango cha juu zaidi na endapo kufikia kuzidi mafuta na gesi nchini humo na hivo kuongeza pato kwa taifa.
Rais Jonathan pia alisema, sanaa hiyo imeonekana kuongeza ajira kwa vijana wengi nchini humo na hivyo inafaa kuungwa mkono ili iweze kutanua wigo wake na kufikia viwango bora zaidi.
Nigeria inafahamika kwa kutengeneza filamu nyingi zaidi lakini zimekuwa zikikosa ubora na viwango vinavyostahili kuwepo kwenye filamu. According to the president, mfuko huo utafunguliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi wa nne na safari hii wanaweza wakatoa filamu zenye ubora zaidi.

No comments: