ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 4, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI


Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani  na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo kwa kuendeleza Lugha na Utamaduni wa Kiswahili. Madhumuni ya hili tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wa Watanzania wanaoishi huku Marekani waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Sherehe zitafanyika 
July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center uliopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wa kiswahili Marekani ya Kaskazini

TEGA SIKIO HABARI ZAIDI ZITAFUATA
-------------------------------------------------------
kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165 Asante

No comments: