ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 20, 2013

“That’s true (ni kweli) Nimemtia Mimba Penny-Diamond

NASIBU Abdul ‘Diamond Platnumz’ amethibitisha madai kuwa mpenzi wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ni mjamzito a.k.a kitumbo ndiii!

Kwa mujibu wa Diamond, ni kweli yeye na Penny ambaye ni presenta wa Kituo cha Runinga ya DTV wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kabla hata ya ndoa waliyopanga siku zijazo.
Diamond alifunguka kuwa tayari amempa mrembo huyo gari la kutembelea huku akimwagizia lingine jipya aina ya Hyundai ix35.

“That’s true (ni kweli) nimemtia mimba Penny, unajua sipendi kusema mpenzi wangu, sasa hivi ni mama watoto wangu. Ni kweli pia nimempa gari kwa sababu ya mizunguko ya kwenda kliniki na nini, nikaona siyo vizuri kwenda kugombea daladala,” alisema Diamond.
Gari hilo jipya aina ya Hyundai ix35 gharama yake inakadiriwa kufikia Sh. milioni 50.

1 comment:

Anonymous said...

haya wee kitumbu mbwii wema alikuwa mjanja hawezi kutiwa kitumbo mbwii bila ya ndoa big up wema