ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 8, 2013

UJUMBE KUTOKA KWA DAYNA KUHUSU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Naitwa Dayna Nyange. Mwanamuziki wa Bongo Freva. Ni Mwanamke wa KiTanzania. naungana na wanawake wengne duniani kote katika kuadhimisha Siku ya wanawake duniani. Nawashauri wanawake wenzangu juu ya kujituma kufanya kaz ili kujipatia maendeleo bila kutegemea wanaume. Naamini wenyewe tunaweza tena bila ata ya kuwezeshwa. Nakupitia siku hii muhimu kwetu naiomba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha inapambana vilivyo juu ya unyanyasaji wa kijinsia tunaoupata wanawake. hasa ubakaji, ukeketaji na mauaji yanayoendelea zidi yetu, tunaiomba serikali ihakikishe kwamba wahusika wa matukio kama hayo wanachukuliwa hatua za haraka ili kukomesha maovu hayo. Pia nijukumu la kila mwanamke na Niwajibu wetu kina Mama pia na jamii kwa jumla kupambana na majanga haya. tushikamane kujiletea. Tupendandane tushikamane WANAWAKE TUNAWEZA By Dayna Nyange.

No comments: