Paroko msaidizi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Joseph Mapunda akiwaosha miguu waumini wa kanisa hilo lililopo Makuburi wakati wa ibada ya Alhamisi Kuu, jijini Dar es Salaam, jana. Picha na Fidelis Felix.
Dar es Salaam: Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam Kardinali Polycarp Pengo jana aliongoza ibada ya Alhamisi Kuu huku kukiwa na ulinzi mkali uliowajumuisha polisi waliovalia sare na wale kawaida, ikiwa ni siku moja baada askofu huyo kulituhumu jeshi hilo kwa kutowajibika ipasavyo.
Askari hao walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili ambao baadhi yao walionekana wakirandaranda eneo la nje ya Jengo la Kanisa la Mt. Joseph ambako ibada hiyo ilifanyika huku wengi walikuwa ndani ya kanisa walikojumuika na waumini wa kawaida.
Haikuweza kufahamika mara moja sababu za kuimarishwa kwa hali ya ulinzi, lakini baadhi ya vyanzo vya habari vilieleza kuwa, hali hiyo imejitokeza kama sehemu ya kujaribu kukabiliana na hali yoyote hasa kutokana na vipeperushi vilivyosambazwa siku za chache zilizopita.
Pengo alikuwa akiendesha ibada ya Alhamisi Kuu ambayo Yesu Kristu alikuwa akifanya ibada hiyo kwa kuwaosha miguu mitume wake.
Ibada hiyo ilifanyika dunia nzima kwani hata Papa Francis alifanya kazi hiyo kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki kwenye Mji wa Vatican, Italia.
Siku chache kabla ya kuingia msimu wa Sikukuu ya Pasaka inayoanza leo kwa Ijumaa Kuu,
vilisambazwa vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe wa kuvuruga ibada za Pasaka , hatua ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kutoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la uvunjifu wa amani.
Ibada ya Sikukuu ya Pasaka kitaifa imepangwa kufanyika mkoani Dodoma.
vilisambazwa vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe wa kuvuruga ibada za Pasaka , hatua ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kutoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la uvunjifu wa amani.
Ibada ya Sikukuu ya Pasaka kitaifa imepangwa kufanyika mkoani Dodoma.
Mwananchi
1 comment:
BWANA YESU ANATUPENDA SANA NDIYO MAANA AKAAMUA KUONYESHA KWA MATENDO KWA KUWAOSHA MIGUU WANAFUNZI WAKE.
WWW.JUMUIYABMM.BLOGSPOT.COM
Post a Comment