ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 17, 2013

MGIMWA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MIKUTANO YA KIPUPWE MJINI WASHINGTON DC

Baadhi ya Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao. Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda pamoja na Kamishna wa Sera Bw. Beda Shallanda.
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya Fedha Bw. Patric Pima.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
kwa picha zaidi bofya read more
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul Mwafongo.


Mikutano ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Augustiao William
Mgimwa ni Gavana mmoja wapo katika mikutano hiyo na Nchi ya Tanzania ni mwanachama katika mikutano hii.

Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Aidha pamoja na mikutano hiyo kunakuwa na semina na majadiliano mbalimbali, mikutano ya waandishi wa habari na matukio mbalimbali yanayohusu uchumi jumla , maendeleo ya kimataifa na masoko ya kifedha ya kimataifa.

No comments: