Dodoma: Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda anatarajia kuongoza maandamano makubwa ya ng’ombe kutoka Lusumo Nyakabanga Mkoani Kagera, hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ili kupinga uonevu na manyanyaso wanayofanyiwa wafugaji.
“Kama watu wanasema ni porojo za Shibuda, basi wasubiri kama hotuba ya Waziri Mkuu haitakuwa na majibu kwa wafugaji, lazima hayo yatatokea kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, hawa nao ni binadamu waambiwe basi kama hawatakiwi Tanzania,” alisisitiza.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi akiwa na uongozi wa wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa ambao wako Dodoma kwa lengo la kuonana na Mawaziri wa Maliasili na Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri Mkuu, ili kufikisha kilio cha wafugaji ambao wanateketezewa mifugo yao na askari wa wanyama pori.
Shibuda alisema kuwa “Katika nchi yoyote duniani hakuna mateso yanayofanywa kwa wananchi wake kama ambavyo inafanyika Tanzania kwa upande wa wafugaji, ni heri ya wakimbizi watakuwa na amani kuliko hawa wanaonekana kama takataka.”
No comments:
Post a Comment