Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mwanachama mpya wa CCM tawi la Mawasiliano, Ulanga, Magdalena Mashinga. Kushoto ni Khatibu na Mwenyekiti wa CCM Moro
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Abeid Mloka aliyetangaza kuhamia CCM, wakati Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa miongoni mwa vijana watano walioamua kuahamia CCM papo hapo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro,
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye Kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kitabu wageni alipokagua uhai wa Chama kwenye tawi la CCM la Ulanga mjini,mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib.
kwa picha zaidi bofya read more
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi la CCM Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro, Francis Kanyali aliyekuwa akisoma taarifa, Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama,
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la wanachama wa CCM kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro, alipofika hapo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM shina la Mawasiliano, Ulanga, mkoani Morogoro, Petro Kabisi akiwatambulisha viongozi wa shina hilo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyetembelea tawi hilo kukagua uhai wa Chama
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ilkiyokuwa ikipigwa na kina mama, kwenye tawi la CCM Nawenge Ulanga, alipowasili kwenye tawi hilo kukagua uhai wa Chama
Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment