Advertisements

Wednesday, April 17, 2013

TWASIRA MBALIMBALI ZA MAANDALIZI YA MSIBA WA BI.KIDUDE

Gari lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab, marehemu Fatuma Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani na kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi yatayofanyika kesho mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanZinews)
Mwili wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika kesho mchana na Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Ndugu, Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarisho ya mazishi yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mrajisi wa Baraza la Sanaa la Zanzibar, Khadija Batashi, akizungumza na waandishi wa habari jinsi alivyoupokea msiba wa msanii mkongwe wa muziki wa taraba nchini, Bi Kidude.
Matayarishi ya mazishi ya msanii wa muziki wa tarab, Bi. Kidude yakiendelea nyumbani kwake Rahaleo, mjini Zanzibar.
Mjukuu wa Bi. Kidude Omar Ameir, akiwasiliana na jamaa kwa ajili ya kuwajulisha msiba wa marehemu Bi. Kidude, baada ya mwili wa marehemu huyo, kuwasili nyumba kwake kwa ajilimatayarisho ya mazishi yatakayofanyika kesho mchana baada ya Swala ya Adhuhuri, ambapo atazikwa Kitumba.
Bi. Maryam Hamdani akilakiwa na Bi. Sihaba wakati akiwasili nyumbani kwa marehemu Bi. Kidude Rahaleo, mjini Zanzibar akiwa na majonzi.  
Waandishi wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi. Kidude, Maryam Hamdan, kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa safari za Bi. Kidude nje ya nchi na katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi wakati wa uhai wake.
Meneja wa Sauti ya BUSARA Zanzibar, Stella Steven, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Zanzibar kwenye msiba huo, kuhusiana na marehemu Bi. Kidude ambaye alikuwa akidhaminiwa na Sauti za BUSARA katika matamasha mbalimbali yaliokuwa yakiandaliwa na taasisi hiyo  ya sanaa, jinsi walivyopokea kifo chake kwa masikitiko makubwa na kuacha pengo katika tasnia ya muziki wa taarab asilia Zanzibar.  
Picha kwa hisani ya Jestina-George

3 comments:

Anonymous said...

Sadly I say. Inna lillahi wa inna ilayhi rajium. May your soul rest in peace the late Bikidude binti Baraka. We shall always love you.

Haji R. Haji. Washington state.

Anonymous said...

inna lillahi waina illahim rajiun ama kweli kwa hakika binadamu hatuna kitu mwisho wetu sote tutakwenda kama alivyokwenda marehemu bi kidude/fatma bakar rahman amlaze mahali pema peponi amin

NY

Unknown said...

Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi Bi mkubwa wetu, alikuwa mwalimu wa mambo mengi hasa kwetu ss akina dada na ameshawaandaa wanawake wengi ambao washadumu na ndoa zao. R.I.P Bi mkubwa wetu Bi Kidude tutakuwa na ww kiroho ck zote za maisha yetu, MBELE KWAKO NYUMA KWETU BIBI YETU. TUTAZIDI KUKUPENDA CKU ZOTE HATA KAMA HATUPO PAMOJA KIMWILI.