Mbio za marathon zitakazofanyika jijini London leo zimeandaliwa huku kukiwa na tahadhari kubwa ya usalama kufuatia mashambulizi ya bomu yaliyozikumba mbio za marathon za Boston nchini Marekani.
Milipuko hiyo miwili ambayo iliwauwa watu watatu na kuwajeruhi wengi zaidi ya 180 mjini Boston Jumatatu wiki iliyopita, imewalazimu waandalizi wa mbio za London kuimarisha mikakati ya usalama katika jitihada za kuwapa matumaini wanariadha pamoja na takribani watazamaji nusu milioni watakaojitokeza kushangilia mitaani.
Polisi zaidi watafanya doria katika barabara itakayotumia kwa mbio hizo.
Serikali ya Uingereza imeahidi kufanya kila iwezalo katika juhudi za kuhakikisha usalama wa wote watakaoshiriki tamasha hilo maarufu.
Wanariadha watavaa vitambaa vyeusi, wakati waandalizi wakisema kuwa euro mbili, na senti thelathini kwa kila mwanariadha atakayemaliza mbio hizo zitatolewa kugharamia waathiriwa wa mashambulizi ya Boston.
Mdimuz Blog
No comments:
Post a Comment