ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 11, 2013

Balozi Seif Ali Iddi Afunguwa Kiwanda cha Maji Safi Amani .


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa hapo maeneo huru amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria kukifungua rasmi Kiwanda cjha maji ya Kunywa cha Super Shine Kinachomilikiwa na Kampuni ya Safari yenye Makao Makuu yake Nchini India.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kufuta hati zote ilizozitowa kwa ajili ya matumizi ya Ardhi ambazo wamepewa baadhi ya watu kwa shughuli za ujenzi au uwekezaji ambapo watu hao wahajazifanyia lolote ardhi hizo kwa kipindi kirefu sasa.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa Kiwanda kipya cha Maji ya Kunywa { Drinking Mineral Water Process Boiling Plant } kinachomilikiwa na Kampuni ya Safari hafla iliyofanyika katika maeneo huru ya Viwanda yaliyopo Amani Mjini Zanzibar.


Balozi Seif alisema kumekuwa na mrundikano wa maeneo kadhaa ya ardhi yalizozunguushwa ukuta ambayo Serikali tayari imeshayagundua na kumuagiza Waziri anayehusika na Ardhi kuwafutia mara moja hati ya usajili wa matumizi wahusika hao.


Alisema tabia hiyo mbaya kwa kiasi Fulani imekuwa ikichangia kuviza maendeleo ya uwekezaji hapa Nchini na kuwakatisha Tamaa watu na makampuni yenye nia ya kutaka kuwekeza Vitega uchumi vyao hapa Nchini.


“ Mimi na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar tumeshakubaliana kukabiliana na tatizo hili sugu, kwani tayari Waziri anayehusika na masuala ya Ardhi ameshaagizwa kufuta hati ya matumizi kwa mtu aliyeshindwa kuitumia ardhi hiyo “. Alitahadharisha Balozi Seif.


“ Wapo watu waliojilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi kwa tamaa ya kuyauza baadaye kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za Serikali. Wanajiuzia ardhi na kusahau kwamba ardhi yote ni mali ya Serikali na ndio yenye uwezo na mamlaka ya ardhi hiyo itumike kwa shughuli gani “. Alionya Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia moja ya sampuli ya chupa ya maji yenye ujazo wa nusu lita ambayo tayari imeshakamilika utayarishaji wake katika kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo Maeneo huru Amani. 
Balozi Seif akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wakishangiria moja ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na kikundi cha sanaa kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda Amani.

wasanii wa Kikundi cha sanaa Zanzibar wakitoa burdani safi katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo amani maeneo huru ya viwanda

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wale wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwanda cha maji ya kunywa hapo amani eneo huru la Viwanda. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri anayesimamia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mh. Omar Yussuf Mzee, Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Nd Salum Khamis na Mmmoja wa Viongozi wa Kiwanda hicho.Kushoto yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwadna hicho Bibi Mala Kalwan na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments: