Tuesday, May 14, 2013

GELLY WA RHYMES APIGWA ROBA NA VIBAKA

Star wa single ya mama ntilie Gelly wa Rhymes usiku wa jana haukuwa mzuri kwake baada ya kuvamiwa na vibaka akiwa njiani kuelekea club bilcanas kwenda kutoa support kwa Hemed aliyekuwa akizindua wimbo wake mpya wa rest of my life.
Taarifa zinasema kuwa vibaka hao walimkaba na kumsababishia majeraha maeneo ya usoni na hawakumfanyia madhara makubwa na hilo lilipelekea kushindwa kufika kwenye show ya mshikaji wake Hemed,na taarifa hii ni kwa mujibu wa mc wa show hiyo iliyofanyika usiku wa juzi club bilcanas ambapo kabla haijafika zamu ya Gelly kuperfome mc alitoa taalifa hizo,TEENTZ inaendelea kufuatilia kujua undani wa mkasa huo.

1 comment:

Anonymous said...

wamemkaba tu bila kumchukulia chochote au kumfanya kitu? habari mbona haituelezei zaidi bwana luke tupe udaku bwana