Taasisi ya Hassan Maajar Trust Yatoa Msaada Wa Madawati Mkoa wa Mwanza
Tarehe 7 Mei 2013 - Mwanza. Taasisi ya Hassan Maajar imetoa masaada wa madawati 250 katika shule za msingi mkoa wa Mwanza.
Zaidi ya wanafunzi 700 katika shule tano za wilaya tano ya mkoa wa Mwanza zimepokea msaada wa madawati yaliyotolewa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Jumla ya madawati 250 yalitolea na taasisi hiyo ikiwa ni kampeni yako ya kupunguza tatizo sugu la upungufu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, ilifanyika katika Shule ya Msingi ya Nyaminjundu, iliyoko Wilaya ya Misungwi. Bwana Shariff Maajar, pamoja na Bi Zena M Tenga kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Engineer Evaristi Ndikilo.
“Ni adimu na mara chache kuona Taasisi za kinyumbani za kiTanzania, kufika hapa mkoani kwetu. Kwa hiyo napenda kutoa shukurani za dhati kwa Taasisi ya Hassan Maajar kwa msaada huu mkubwa na wenye thamani utakaochangia kuboresha elimu katika Mkoa wetu wa Mwanza”, alisema Engineer Ndikilo. “Kama mikoa mengine ya nji yetu, ni wilaya na halmashauri za vijiji ambako msiaada kama hii inaitajika kwa wingi na ni kweli kati ya changamoto nyingi zinazowakabili watoto wetu, moja wapo ni hili la upungu wa mazingira bora ya Elimu, kwa hiyo tunawashukuru Hassan Maajar Trust kwa kuzingatia hizi changamoto na kwa kuufikiria mkoa wetu wa Mwanza”, aliongeza.Huu ni msaada wa tatu chini wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) mkoa wa Mwanza ni mko watatu kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011. Hadi sasa Hassan Maajar Trust imekabidhi jumla ya madawati 1,194 kati ya madawati 1,764; Njombe (680), Singida (264), Mwanza (250). Mikoa itayofawatia ni Lindi na Rukwa. Garama za madawati haya ya mkoa wa
Mwanza ni jumla ya Tsh 22,500,000.
“Lengo letu hususan ni kujitahidi kuhakikisha Taasisi yetu inaboresha mazingira ya kusomea watoto katika shule zetu Tanzania”, alisema Zena M Tenga Mkurugenzi Mtendaji. “Tunatarajia na tunalenga kuhakikisha kuwa kampeni yetu ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto wengi iwezekenavyo na pia tutaendelea kuhamasisha jamii, taasisi tofauti na mashirika tofauti kuendelea kutuunga mkono ilituweze kufanikisha malengo yetu”, aliongeza.
Kuhusu
Hassan Maajar Trust
Taasisi ya Hassan
Maajar Trust
imeandikishwa kama kampuni au NGO isiyo na hisa na yenye kudhaminiwa na kufanya
kazi za hisani bila faida. Lengo kuu la Taasisi ya Hassan Maajar Trust ni
kuboresha mazingira ya elimu katika shule za Tanzania.
Kwa
maelezo zaidi tembelea: www.hassanmaajartrust.org
| www.hassanmaajartrust.blogspot.com
No comments:
Post a Comment