Kama anamfahamu msanii wa muziki wa kizazi kipya Mzungu Kichaa katika gemu basi
hivi sasa kuna mzungu mwingine anayeitwa Badawi, ambaye ameibuka nchini Tanzania
kuwashika mashabiki wa miondoko hiyo ambapo licha ya kufokafoka jamaa anafanya
pia miondoko ya reggae.
Badawi Poa mzaliwa wa nchini Ujerumani ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliye chini ya label ya Kama Kawa Records, ambaye kwa uzoefu wake wa miezi minane Tanzania, ameamua kuandika ngoma kuhusiana na hali halisi ndani ya daladala Tanzania ambapo wasafiri hulazimika kujaa hadi kusimama na kushikilia bomba ndani ya gari ili kuweza kufika katika mizunguko yao tofauti tofauti.
Msanii huyu ameipatia kazi hii jina 'Shika Bomba' na Jumamosi hii anatarajia kuiachia video yake akiwa na matumaini makubwa ya kufanya poa katika game ya bongo flava Tanzania. Inspiration yake kubwa ikiwa ni wasanii kama vile Professa Jay, Lady Jay Dee na wengineo.

1 comment:
kazi iko wabongo kazi ipo mtakiona sasa wenzenu wanakukamuliyeni nyinyi mnalala usingizi wa kufaa
badawa poa mwanangu kamu kamu bongo kuna maziwa ya bureee ya ngombe dume
Post a Comment