Mwanamziki Qute Kaye wa nchini Uganda amejitokeza kukanusha uvumi ulioenea
wiki hii kwenye mitandao ya jamii, kuwa amefariki dunia baada ya kuugua.
Msanii huyo anayejulikana kwa vibao vyake kama Ginkese, Gwendota, Njagala
Omuwala, pia amekanusha kuumwa.
Hii si mara ya kwanza msanii huyo aliyeibuka mwaka 2007 na albamu yake
Ginkese iliyotesa sana klabu, baa na redioni, kuzushiwa kifo na safari hii uvumi
huo ulikuzwa mno.
No comments:
Post a Comment