Friday, May 3, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YAFUTWA, MITIHANI KUSAHIHISHWA UPYA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (kushoto), akiwa bungeni mjini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Sengerema,William Ngeleja.

HABARI zilizotoka bungeni mjini Dodoma muda huu ni kwamba matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne kwa mwaka jana imesomwa leo bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema sababu zilizosababisha wanafunzi hao kufeli ni pamoja na upungufu wa waalimu, mazingira magumu ya kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) uliotumika bila kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu.

Kutokana na sababu hizo, matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya.

2 comments:

Anonymous said...

Hiki ni kichekesho cha mwaka!!! Kwani kufeli kumesababishwa na makosa ya usahihishwaji wa mitihani? Hii si moja ya sababu ambazo tume imezitaja. Nadhani huu sasa ni mchakato wa kupika matokeo ili kusetiri uso wa serikali yetu ambayo imeonyesha udhaifu mkubwa katika kukuza kiwango cha elimu nchini. Shame on you Mr. President and your incompetent cabinet!

Anonymous said...

Kula tano anon wa kwanza! U said it all!