Advertisements

Friday, May 3, 2013

Wazee wapewe haki kuoa, kuolewa, asema Mbunge


"Swali hilo lilizua kicheko kwa wabunge ndani ya ukumbi, huku baadhi wakishangilia na kupiga makofi kwa nguvu kuonyesha kuguswa na jambo hilo"
Kitendo cha kutowapa nafasi wazee waoane ni kuwanyima haki yao ya msingi na hivyo ni uvunjifu wa haki za binadamu
Dodoma. Mbunge wa Ole,Rajab Mbarouk Mohamed (CUF), ameitaka Serikali iweke mikakati maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wazee wanaoishi katika makambi maalumu ili nao waweze kuoa na kuolewa.

Wakati mbunge huyo akilalamikia suala hilo, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga (Chadema), alihoji ni kwa nini Serikali inaacha wananchi wa hospitali za Mang’ula wanalala wodi moja wanaume na wanawake jambo ambalo ni hatari.
Alitoa kauli hiyo katika swali la nyongeza kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati Naibu Waziri wa wizara hiyo,Dk Seif Rashid alipokuwa akijibu swali kuhusu Kambi ya Wazee wa Kilima katika Mkoa wa Kagera.
Swali hilo lilizua kicheko kwa wabunge ndani ya ukumbi, huku baadhi wakishangilia na kupiga makofi kwa nguvu kuonyesha kuguswa na jambo hilo.

Hata hivyo, Naibu Waziri, Dk Rashid alikiri kuwa ni haki ya watu hao kupata wenza kama ilivyo kwa wengine kama watakuwa na nguvu bado za kufanya hivyo.
Aliwataka wabunge na jamii kushirikiana katika kuwasaidia wazee ili waweze kupata wenza pindi watakapohitaji .

Kuhusu wananchi kulala wodi moja wanawake na wanaume Morogoro, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Aggrey Mwanri alisema jambo hilo litafuatiliwa.

No comments: