Sunday, May 19, 2013

MCHUNGAJI PETER MSIGWA MIKONONI MWA POLISI

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa.

Taaarifa kutoka Iringa zinasema mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amekamatwa na jeshi la polisi na yuko chini ya Ulinzi.Mchungaji Msigwa amekamatwa kwa amri ya Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Michael Kamuhanda kwa madai kwamba anawaunga mkono wafanyabiashara ndogondogo wa manispaa hiyo 'Machinga' wanaopambana na polisi wanaowakataza kufanya biashara mjini.
Mchungaji Msigwa amekuwa mtetezi mkubwa wa wafanyabiashara ndogondogo kiasi kwamba kila anapoonekana maeneo ya manispaa hiyo hujikuta gari yake ikisukumwa na Machinga hao. Kabla ya kukamatwa, Mchungaji Msigwa alikuwa katika harambee iliyokuwa inaendesha na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Chuo Kikuu cha Tumaini.-GPL

3 comments:

Anonymous said...

Jamani mbona siku hizi wabunge wanawekwa ndani kuliko hata hao waalifu uzalendo huko wapi? Mbona baba wa taifa hakufanya hivyo.

Anonymous said...

Mzalendo wa kwanza ni yule anayefuata sharia halali za nchi hata kama anaona hazimfai yeye kwa wakati husika. Mzalendo wa kweli ni yule anayetumia jukwaa lolote alilokabidhiwa bila kuwaghadhibisha wale aliopewa jukumu kuwaongoza ili nao bila kutumia muda kutafakari hali halisi na kwa mwongozo wa busara zaliwa hali halisi waweze kufanya uamuzi makini ambao umejengeka katika misingi tuliojiwekea wenyewe kuepusha nchi kutokana na janga la vurugu. We are at the split point where peace which is holder of development, is threatened by individual popularity mongering. This is sad we used to have a common enemy but now we have a devided front - We are done! There will be no Tourism,No Foreign Investment if this is how we ride the blessings we had. God Bless Tanzania!!

Anonymous said...

Again, wakati Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uhasama wa kidini, hawa hawa viongozi badala ya kuisaidia serikali ambayo wao ni moja ya mihimili yake ya uongozi wao wanatafuta chumba cha pekee wakitumia upeo wao mdogo katika kujua kuwa dola hiyo wanayo itaka iwalinde wao ndiyo hiyo hiyo ambayo wanaichagiza badala ya kuitumikisha kwa mwelekeo wa uwajibikaji husu ili kupata utatuzi husu wa matatizo yanayoikabili Tanzania yetu. Si tu madini na Maliasili ni laana kwa Taifa letu bali hata Uwelewa mfupi wa masuala hayo pia ni laana maana nchi yoyote kama ambavyo haitawaliwi na jasba pia haitawaliki kwa visasi tengenezwa na hata kutofahamu au kutokuwa na uwezo wa kupembua lipi la manufaa na lipi la binafsi kwa mwendo wa kuwasahau wale waliotupa majukumu kuwawakilisha maana pengine hata wabunge hawajui kuwa mbunge kama mwanasiasa si mpigania haki iliyotofauti na ili siasa iliyomwezesha kuitwa mbunge. Kuna siasa za Barabarani na siasa za Bungeni. Kamwe haziwezi kulazimishwa kuwa zote ni sawa na zinakwenda sambamba. Nadhani Nchi ina sharia na kama sharia hazifai, basi njia halali na ya busara itumike kuzirekebisha na si vinginevyo. Sisi sote ni mashahidi kuwa Tanzania yetu inaangamia wakati tunaiona. Tutajihukumu wenyewe kwa hili.