ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 7, 2013

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
kwa picha zaidi bofya read more
Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013. PICHA NA IKULU.

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kwa hili...NAKUPONGEZA Mhe. Rais

Anonymous said...

Safi sana mheshimiwa rais. Sisi wakatoliki huwa hatuna makuu. Tumewasamehemwote waliohusika. Tunawaombea kwa Mungu na tutawapenda milele.

Anonymous said...

Kwanini???? Tanzania this how other countries fell apart, we are so much better than this!!!!! Amani jamani Ndio mbegu ya mafanikio.... Or we will all be refugees!!

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto unampongeza Raisi kwa kuwa kwenye matukio au kwakuzuia matukio haya? Sijaelewa pongezi yako hasa ni ya nini? Personally nawapongeza hawa masista na mapadre kwakuwa na moyo wakusamehe. Maana kwa marudio ya matukio haya lazima upate hasira na watu waliokabidhiwa dhamana ya kulinda amani ya nchi. Lakini nawaona kweli wanatimiza ile ya kusamehe mara saba sabini.