Saturday, May 25, 2013

SHEREHE YA KICHURI YAFANA

 Kichuri kikiwa tayari kwenye Shere ya Kichuri inachowakutanisha Wakurya na watu wote wa mkoa wa Mara pamoja na  watani wao na marafiki zao wa Marekani hapo Ellicott City.
Angalia Video ya Ritungu linavyochezwa hapo chini.

 Wakurya wakicheza Ritungu huku watoto wao nao wakijumuika nao.
Kadogoo akifuata nyayo.
Wakurya na marafiki zao wakibadilishana mawili, matatu.
 Mahanjumati yenye madoido ya mbuzi aliyekorezwa kwa kichuri yakiendelea. 
 Akina mama wa kikurya wakipata picha ya pamoja kwenye Sherehe ya Kichuri ya kwanza ya aina yake. Sherehe hii itakuwa ikifanyika Marekani kila mwaka.
Kulia ni mtani wa Wakurya, Edgar Tibaikweitira, akielekezwa kwenye kona ya hema kilipo Kichuri. Kushoto ni wenyeji wa sherehe mwaka 2013 Eda na mumewe Vicent.
 Ilikuwa furaha kubwa na fahari kwa Watanzania hawa kujikumbusha mila na desturi za kikwao.
 Vicent akipiga porojo na mama wa kikurya, Rose, ambaye hakuamini macho yake alipokumbana na vitumbua vya Uswahilini kwenye sherehe ya kikurya.
 Baadhi ya wageni wa Wakurya kutoka Washington DC, Ali na Mike waliofika kwenye Sherehe ya Kichuri.
Mama Matinyi akimnyanyua mwanae Ghati kwa furaha.
kwa picha zadi bofya read more

 Nyama choma ikiendelea huku mgeni wa Wakurya, Saria, akishuhudia. Anayechoma nyama ni mzee wa kikurya, Waigama, huku mwenyeji Eda akiionja nyama ya mbuzi.
Tifa, toto la kikurya, likindaa mahanjumati
 Kutoka kushoto ni Elvis Saria, Mobhare Matinyi na Edward Waigama wakipatapata nyama choma na kichuri kinachoendelea sasa hivi Ellicott City.
 Familia ya Matinyi wakiendelea na nyama choma na kichuri kinachoendelea Ellicott City
 Juu na chini Watoto wakicheza. Hapa juu ni Mwita akimwendesha Chacha, watoto wa kikurya walioshinda michuano ya karate nchini Marekani hivi karibuni.
 Grace Saria katika pozi ya kutengeneza picha ya albam yake ya muziki, Grace anakipaji sana cha kuimba siku si nyingi utamsikia akiimba.
Lulu Waigama akiwa na kadogoo wake. Mtoto huyu wa kikurya alivunja rekodi ya kula nyama nyingi za mbuzi kwa watoto wa umri wake.

4 comments:

Anonymous said...

Hivi vikundi mbona vingi hata wachaga tukianza mtasema nini ?? Haya wachaga mkae tayari

Anonymous said...

Mtoto wa nyoka ni nyoka. Huyo mtoto simshangai ni kama baba yake, tu!

Anonymous said...

nimeipenda sana hii sherehe mila muhimu iendelezwe popote ulipo watoto wanahitaji kujijua identinty yao tusiwe kama wamarekani hawana hata identity wala mila big up wakurya mmefungua ukurasa na nyie makabila mengine tufate nyayo msikalie maparty yasiyo na mafunzo yoyote hapa watoto wanajifunza mila na tamaduni hata wakiishi ulaya bado wanajua mambo ya kwao walikotoka angalau mara moja kwa mwaka hiyo miezi hongera sana watani zangu wakurya
koku

Anonymous said...

Ah, Wakurya wenyewe Feki hao. Wange-rireta-riafande Marwa na Matiko- weweee- rione rinareta fujoo.rikamate -unasikia 'pot' (homeboy kwa kikurya). eti kira siku hana apetaiti-(JKT)muombe rafiki yako,arrah.