Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
HOTUBA YA JAJI WARIOBA
HOTUBA YA JAJI WARIOBA
Mhe. Dkt Mohammed
Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
• Mhe. Mizengo
K. P.
Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
• Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
• Mhe. Balozi
Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,
• Mhe.
Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
• Mhe. Abubakar
Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar,
• Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
• Mhe. Othman Masoud
Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
• Viongozi wa Vyama
vya Siasa,
• Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba,
• Ndugu Wananchi,
• Wageni Waalikuwa
• Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.
1.0. UTANGULIZI
Ndugu Wananchi,
1
leo ya kuzindua
Rasimu ya Katiba.
pia, niwashukuru
ninyi nyote mliohudhuria halfa
hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa
Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa
mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa
Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu
wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa
miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake
kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo
ilikuwa Mei 2,
2012.
Tume iliandaa ratiba
ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana
na ratiba hiyo
Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano
kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba,
2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga.
Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao
1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537
walitoa maoni ama kwa
mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume
pia ilipata maoni ya
wananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano
ya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua
kupitia Masanduku ya Barua ya Tume,
Mitandao ya Kijamii
ya barua pepe; facebook
ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala
mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.
Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika
jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali,
taasisi za dini,
wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia
na kadhalika. Makundi zaidi ya
160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya viongozi wa juu
wa Serikali walioko
madarakani na waliostaafu. Kwa jumla viongozi
43walitoa
maoni.
2
wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni tuliyopata
yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa,
tulitambua
umuhimu wa kuongeza
muda hadi mwisho wa mwezi
Mei, Maoni ya wananchi
yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana. Aidha,
baadhi ya maoni yaligusia masuala
ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji. Tulifanya
uchambuzi makini na wa
ndani wa maoni hayo na kazi hiyo tumeikamilisha na rasimu
imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya kuizindua, ambapo Wananchi
watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya Tume, napenda kutaja maeneo
machache tu ambayo tunayapendekeza.
2.0. IBARA
ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA
Ndugu Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina
ibara 152. Tume ilifanya jitihada
kubwa sana kuandaa
rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini
katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu
ya
Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.
3.0. MISINGI
MIKUU YA TAIFA
Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni
Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na
inastahili kubaki kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza
misingi mingine mitatu ya Usawa, Umoja na
Mshikamano. Hivyo, Tume
imependekeza
Katiba iwe na Misingi Mikuu
saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki,
Udugu, Usawa, Umoja, Amani na Mshikamano.
4.0. TUNU
ZA TAIFA
Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National
Values).
Wananchi wengi walitoa
maoni kwamba Katiba
itaje Tunu za Taifa.
Tume
imependekeza
Tunu zifuatazo zitajwe
ndani ya Katiba.
Tunu hizo ni;- Utu,
3
Kiswahili.
5.0. MALENGO YA TAIFA
Tume ilipozunguka nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu
malengo ya
taifa. Walitaka
Katiba ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto
yao ya
Tanzania ya kesho na kesho kutwa.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna sura
nzima inayohusu Malengo
mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli za
Kiserikali na Sera za Kitaifa.
Rasimu ya Katiba inaeleza
kuwa Malengo ya Kitaifa
yaliyoainishwa
ndani ya Rasimu yatakuwa
ni Mwongozo kwa Serikali,
Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa, Taasisi na Mamlaka nyingine,
na kwa
kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri Masharti ya Katiba au Sheria
nyingine za
Nchi.
Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa
mpangilio wa kuonesha malengo
ya kisiasa, kiuchumi,
kijamii, kiutamaduni,
kimazingira na sera ya mambo ya nje. Malengo hayo yameingizwa kwenye
Rasimu ya Katiba.
6.0. VYOMBO
VYA
KIKATIBA
Wananchi walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba na
kuingizwa kwenye Katiba
ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wa
majukumu yao. Tume imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vya
Kikatiba; Tume ya Uhusiano
na Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, Kamati
Maalum ya Makatibu Wakuu na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na
Usalama la Taifa, Tume Huru ya Uchaguzi,
Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume
ya Utumishi wa Umma, Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za
Binadamu
na Utawala Bora
4
7.0. MAADILI
YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI
Wananchi wengi pia walizungumzia kwa upana sana kuhusu
maadili na miiko ya
Viongozi, kwa kuzingatia maoni ya wananchi Tume inapendekeza maadili
ya
viongozi wa umma, pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba.
Tume pia imependekeza kuwa Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume
yenye mamlaka makubwa
ya kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja
miiko ya
uongozi.
8.0. HAKI ZA BINADAMU
Kuhusu haki za binadamu wananchi
walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe na
vikwazo visivyo vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko
katika baadhi ya haki za
binadamu kwa madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni kuhusu
uhuru wa mwananchi
kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwamba
vikwazo vilivyowekwa kuzuia
mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine
Tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe
kwenye Katiba ikiwa ni pamoja
na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za
Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na
Kujifunza, Haki ya kupata habari,
Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari na
kadhalika.
9.0. URAIA
Wananchi wengi walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba.
Tume imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya
Muungano na haki zake.
10.0. MIKOPO NA DENI
LA TAIFA
Ndugu Wananchi,
Wananchi walizungumzia
suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa
utaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa kuzingatia
5
Bungeni kuhusu Mikopo
kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba yake na matumizi
ya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.
11.0. MFUMO WA UTAWALA
Kuhusu utawala, Tume inapendekeza Tanzania
iendelee na mfumo wa Jamhuri kwa
maana ya nchi inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi wa
Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
12.0. UCHAGUZI
WA RAIS
12.1. Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombea
Urais. Baadhi walipendekeza mtu akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia na
sifa ya kugombea
Urais. Umri wa mtu kuruhusiwa kupiga
kura ni miaka 18.
Wengine walipendekeza umri uliopo kwenye Katiba
wa mtu kugombea Urais,
yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea, uendelee
kubaki kama ulivyo.
Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea
Urais uwe miaka 35 au
miaka 50 na
kuendelea.
Tume imeyachambua maoni yote hayo,
ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za
Nchi zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Marais
katika Nchi mbalimbali
Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea
wa nafasi
ya Urais kuwa
na umri chini ya miaka 40.
Wengi walioomba kugombea
nafasi hiyo walikuwa
na umri wa miaka
40 au zaidi.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza Rais
aendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeomba
urais asiwe
chini ya miaka 40.
6
mgombea mwenza kwa
utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tume
imependekeza
Mgombea Urais anaweza
kupendekezwa na Chama cha
Siasa au kuwa Mgombea Huru.
Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa
mshindi iwapo atakuwa
amepata kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura
zote zilizopigwa.
Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa
Mahakamani, lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaoweza
kufungua kesi ni wagombea Urais.
Aidha, ni Mahakama
ya Juu pekee ndiyo
itakuwa na Mamlaka na uwezo wa kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya
uchaguzi wa Rais na shauri lazima liamuliwe
ndani ya mwezi mmoja, yaani siku
therathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwa
mshindi au kuthibitishwa na Mahakama.
13.0. MADARAKA YA
RAIS
Ndugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba,
Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa
ngazi za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo
vingine katika
uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge
litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya
watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo
Bunge litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe
chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi
na Usalama la Taifa, ambalo kati ya
7
ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu
Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais
kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.
14.0. KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi,
inapendekeza Rais abaki na kinga kama
ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
15.0. IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa
Rais aunde Serikali
ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na
tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri
hawatahudhuria vikao vya Bunge
isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi
kwenye kamati za Bunge.
16.0. BUNGE
Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa
na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa
kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu
wenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na
mwingine
mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa
Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge
wake.
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata
hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa
kipindi
chake.
Inapendekezwa
pia kusiwepo na uchaguzi
mdogo isipokuwa kama nafasi
inayokuwa wazi inatokana
na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi
mdogo kujaza
8
basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe
Viongozi wa vyama vya Siasa.
17.0. TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya uchambuzi
wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume
inapendekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza
sifa za wajumbe
wa Tume Huru ya Uchaguzi
ziwekwe kwenye Katiba.
Wajumbe wa
Tume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa
zilizoainishwa
ndani ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na
Kamati ya Uteuzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine
sita ambao ni Majaji
Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri
ya
Muungano, Maspika wa Mabunge wa nchi Washirika
na Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za
Binadamu.
Kamati ya uteuzi
itapendekeza majina ya watu wanaofaa
kwa Rais ambaye atateua
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi
wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa
tume ya uchaguzi.
Inapendekezwa
Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi,
kura ya maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.
18.0. MAHAKAMA
Kuhusu Mahakama inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme
Court) Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani
watateuliwa na Rais
baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
19.0. MUUNDO WA MUUNGANO
9
Suala la muundo wa Muungano ndilo
lililokuwa gumu kuliko masuala
yote.
Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja
na kwamba
hadidu za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya
wananchi walitoa maoni kwamba
Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni
hayo. Licha ya kwamba waliotaka kuvunjwa muungano
walikuwa wachache sana,
Tume ilichambua sababu walizotoa na kuridhika
kwamba hazikuwa na uzito.
Wananchi walio wengi walitaka Muungano
uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza
Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili,
Serikali tatu, Serikali nne na muungano wa
mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa
na uzito, kwa hiyo
Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Serikali
moja walikuwa wachache
lakini sababu zao
zilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni changamoto
kubwa kuwa
na Muungano wa Serikali Moja
Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi
(hasa wananchi
wa Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana
wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa lakini
hakukuwa na mazingira
ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume iliona
kuna changamoto ya muungano kuvunjika
ingawa waliotoa maoni walisisitiza
muungano
ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Tanzania
iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali
mbili
walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi hili
walipendekeza
mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini
ya Tume ilionyesha
kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.
Wananchi waliopendekeza muundo
wa Serikali tatu walikuwa
wengi kuliko makundi
yote. Sababu
zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi
na nzito.
Pamoja na maoni ya wananchi
Tume ilirejea sababu
za kupendekeza muundo huu
zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbali
10
Serikali tatu. Yaani Serikali
ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
20.0. ORODHA YA MAMBO YA
MUUNGANO
Ndugu Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano
yawe 7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya
muungano yanayopendekwa ni:
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
3. Uraia
na Uhamiaji
4. Sarafu na Benki Kuu
5. Mambo
ya Nje
6. Usajili
wa Vyama vya Siasa
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo
ya Muungano.
21.0. BENKI KUU
Kwa kuwa Tume imependekeza Muungano
wa Shirikisho kutokana
na uzito wa maoni
ya wananchi. Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
itakayokuwa na wajibu wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigeni
na Benki za Washirika wa Muungano.
11
Kutokana na pendekezo la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu,
inapendekezwa
kuwepo kwa Benki zitakazokuwa
na jukumu la kutunza akaunti
ya
fedha za Serikali
za kila Mshirika
wa Muungano na kuzisimamia benki
za biashara
katika mamlaka
zao.
23.0. BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE
RASIMU YA KATIBA
23.1. Serikali
ya Majimbo
Ndugu Wananchi,
Tume ilipokea maoni
kuhusu mambo mengine
muhimu ambayo hayamo katika
rasimu hii. Moja ya mambo hayo ni Serikali za Majimbo.
Tume ilichambua
maoni na sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini
Tume
ilibaini changamoto nyingi na ikaamua
kutopendekeza muundo huu.
Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa
Serikali Tatu, ilionekana ni dhahiri
kuongeza ngazi nyingine
ya Serikali ingeleta
gharama kubwa. Serikali
nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo,
Mabaraza ya Mawaziri
na Mabunge na gharama yake
ingekuwa kubwa.
Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya
Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi
ya maeneo na
ukabila. Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha
nchi kwenye utawala
utakaoigawa nchi kwa misingi
ya ukabila, udini
na ukanda na kuzigawa rasilimali za taifa kikanda
na hivyo kuleta
tofauti kubwa ya kimaendeleo katika
nchi.
23.2. Mahakama ya Kadhi
Ndugu wananchi,
Jambo la pili ni mahakama
ya kadhi. Tume ilipokea
maoni mengi kuhusu suala
hili. Baadhi
ya wananchi walitaka mahakama ya
kadhi iingizwe kwenye Katiba na
12
Serikali Tatu, Tume
iliona kuwa Mahakama
ya Kadhi siyo suala la
Muungano na imeliacha ili lishughulikiwe
na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala siyo
kuwapo au kutokuwapo kwa
mahakama ya kadhi.
Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwa
katika Katiba. Zanzibar kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenye
Katiba ya Zanzibar. Kwa kutumia uzoefu huo hata Tanzania Bara inaweza
kupata
ufumbuzi wa suala hili.
23.3. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
Jambo la Tatu ni Kuwepo
au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa na
Wilaya. Baadhi ya Wananchi
walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo,
wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kuwepo lakini
wachaguliwe na wananchi na waengine wakasema
wawepo na waendelee
kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu suala hili na kuamua
kwamba siyo suala la Muungano
na kwa kuwa Muundo wa Muungano
imependekezwa
uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona suala la uwepo au
kutokuwepo na namna
ya upatikanaji wa Wakuu
wa Mikoa na Wilaya
lishughulikiwe
na Washirika wa Muungano.
23.4. Serikali za Mitaa
Kuhusu Serikali za Mitaa, Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi
kuhusu
kuziimarisha
Mamlaka za Serikali
za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili
wa
kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hili
na kuamua kwamba
siyo jambo la Muungano na hivyo, litashughulikiwa
kwenye Katiba za Washirika wa Muungano.
23.5. Uraia wa Nchi mbili
Ndugu Wananchi,
13
mbalimbali kuhusu kuwekwa
kwenye Katiba suala la Uraia
wa nchi mbili. Baada
ya kufanya uchambuzi
kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba
na yapi
yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba
bali kwenye Sheria
inayohusu jambo husika,
Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi
mbili linaweza kuwekwa
kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye
Katiba. hii ni kwa sababu kutokana
na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo
linaweza kubadilika wakati
wowote na hivyo likiwa kwenye
Katiba linaweza
kuifanya Katiba
kubadilishwa mara kwa mara.
24.0. MWISHO
Naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwa
kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoa
maoni na kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili na
kuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya ambayo
itaakisi
ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa
shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:
1. Kwa
kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima
2. Kwa
kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,
3. Kwa kutokuingilia Uhuru wa Tume wakati wa Utekelezaji wa Majukumu
yake na
4. Kutoa Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini
na Waadilifu ambao
wameunda
Sekretarieti ya Tume.
Ndugu Wananchi,
14
Shukrani za pekee ziwaendee:
1. Wakuu wa Mikoa,
2. Wakuu wa Wilaya,
3. Wakurugenzi / Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4. Makamanda wa Polisi wa
Mikoa na Wilaya,
5. Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.
Kwa kuisaidia Tume kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru
Asasi za Kiraia, Taasisi,
Jumuiya za Kidini,
Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbali
kwa namna walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika
kutoa maoni.
Mwisho ingawa
siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa Wananchi na
katika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato
wa Mabadiliko ya Katiba.
Nachukua nafasi
hii kuwaomba Wananchi
kupitia Mabaraza ya Katiba
ya Wilaya,
Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu
wenye Malengo yanyofanana
kushiriki vyema, kwa umakini,
utulivu na kwa amani katika hatua hii ya kuipitia,
kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.
Tume imekuwa ikithamini na itandelea kuthamini mawazo na maoni kutoka kwa
Watanzania wote.
Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
SASA NAKUOMBA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS UIZINDUE
RASMI
RASIMU YA KATIBA
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment