ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 23, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA KIKAO CHA SMZ NA SMT MJINI DODOMA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Kikao cha SMZ na SMT, kinaochofanyika Dodoma Hoteli, leo Juni 23, 2013. Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, na (kushoto) ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd. 
Mawaziri washiriki katika Kikao hicho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo ameongoza Kikao cha SMT na SMZ, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Hoteli, mjini Dodoma, leo Juni 23. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Idd, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samih Suluhu pamoja na washiriki wa kikao hicho Mawaziri kutoka serikali zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar.
 Juu na chini Mawaziri washiriki katika Kikao hicho
Kwa picha zaidi bofya read more

No comments: