ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 26, 2013

TENDWA AAPA KUUFUTA USAJILI WA CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa, amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta. 
Tendwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp kuhusu hatua zitakazochukuliwa... 

Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu. 

Source :Jamiiforum

3 comments:

Anonymous said...

Asante mheshimiwa TENDWA, ukiwa kama kiongozi wetu, sisi tulioko huku chini masikio yetu yanalenga kupata habari njema, na hasa katika jukwaa la siasa ambalo mara nyingi likishaingiliwa na kauli zisizoridhisha je unategemea nini kinachowezatokea kwa wananchi wapiga kura! Ni vizuri tuangalie kauli tunazotoa kuepusha umwagaji damu kama tunavyoona duniani!! Mungu uendelee kuiangalia Tanzania na watu wake.

Anonymous said...

What if not CHADEMA but CCM was the one involved, will he do the same? He needs to shut up his mouth and do his job right.

Anonymous said...

Tunataka ufafanuzi! Wakifanya CCM ( ambao wanaweza kuwa wamehusika) hatakifuta kwa sababu wanambeba, lakini ikiwa CHADEMA hata kwa kuhisi atakifuta....Huyu mzee naona haelewi anachofanya.