ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 3, 2013

IMEKAAJE HII SERIKALI YAZUIA UJENZI WA UWANJA YANGA

Na Khadija Mngwai
UONGOZI wa klabu ya Yanga umeibuka na kusema kuwa umelazimika kusimama kuanza ujenzi wa uwanja wao mpya kufuatia kusubiri majibu ya serikali.
Yanga ipo katika mikakati ya kuujenga uwanja wake wa Kaunda ili uweze kuwa wa kisasa zaidi na kuwa katika nyasi bandia ambapo awali walieleza kuwa wangeanza ujenzi mwezi Juni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema zoezi hilo la ujenzi wa uwanja kwa sasa limesimamishwa kufuatia kusubiri majibu ya serikali kutokana na kuomba nafasi ya kuongeza eneo la uwanja huo.
“Kwa sasa tumesimamisha zoezi la ujenzi wa uwanja hadi hapo tutakapofanikiwa kupata majibu kutoka serikalini ambapo tumepeleka barua ya maombi Wizara ya Ardhi kwa lengo la kuuongeza.
“Si unajua kuna eneo ambalo tumeliomba serikalini ili tuweze kuuongeza, lakini hadi sasa bado hatujajibiwa, naamini tukipata majibu tu tutaanza mara moja zoezi hilo.
“Mara tutakapokamilisha taratibu zote na kupatiwa majibu tutaweka wazi kila kitu kwa umma na ndipo tutakapoanza mchakato mzima wa ujenzi,” alisema Kizuguto.
Yanga miezi kadhaa iliyopita ilitangaza kujenga uwanja mpya ambao utachukua mashabiki 40,000.

No comments: