Jaji Mstaafu Thomas Mihayo
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imewafungia kwa mwaka mmoja wakandarasi 33 kwa kujihusisha na rushwa wakati wakandarasi sita kati yao walipokea malipo kwa kazi hewa.
Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum kufungua warsha ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi jijini hapa.
Alisema kati ya wakandarasi sita waliopokea malipo kwa kazi hewa, watatu kati yao wamerudisha fedha hizo na wameruhusiwa kuendelea na kufanya kazi.
Hata hivyo, alisema suala lao limepelekwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), yenye mamlaka ya kuwachukulia sheria.
Alisema wakandarasi wengine watatu ambao hawajarudisha fedha hizo, wanaendelea kufungiwa.
Jaji Mstaafu Mihayo alisema adhabu hiyo imeanza kuleta nidhamu kwa wakandarasi wengi tofauti na awali wakati mamlaka hiyo ilipoanza ilikuwa ikisuasua.
Akieleza zaidi kuhusu vitendo vya rushwa kwa maofisa wa mamlaka hiyo, alisema hatua mbalimbali zinachukuliwa dhidi yao na wale wanaobainika kuhusika adhabu inayotolewa kwao ni kuachishwa kazi na sio kuhamishiwa sehemu nyingine na kufunguliwa mashtaka.
Akifungua warsha hiyo, Naibu Waziri Saada alisema suala la manunuzi ni eneo pana na linahitaji usimamizi wa hali ya juu.
Aliongeza kuwa manunuzi ni suala nyeti ambalo linahitaji uadilfu wa hali ya juu kwani watu wengi wanafanya udanganyifu katika eneo hilo.
Alisisitiza umuhimu wa kuwachukulia hatua wote wanaokiuka taratibu na sheria za manunuzi.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Ramadhan Mlinga, alisema mamlaka yake inatarajia kufungua ofisi mikoani ambapo kwa mwaka huu watafungua ofisi mkoani Dar es Salaam na Arusha na baadaye katika mikoa ya Mwanza, Dodoma na Mbeya.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment