Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, ameshangazwa na kitendo cha kupokelewa na mbwa na rundo la magari ya polisi, huku farasi wakiranda randa katika Uwanja wa Ndege wa Arusha
alikoshuka akitokea jijiji Dar es Salaam kwa matibabu.
Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa katika ofisi za mkoa za chama hicho baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara.
“Yaani Polisi wanazuia wapiga kura wangu wasinipokee mimi na matokeo yake wanajaza uwanja mbwa, magari na farasi ndio wanipokee kitendo hiki kimenisikitisha sana,” alisema Nassari.
Nassari alisema alikuwa Dar es Salaam akipata matibabu baada ya kupigwa kwenye harakati za uchaguzi kwenye Kata ya Makuyuni, WilayaMonduli.
Alisema mara aliposhuka uwanjani na kuona kundi kubwa la polisi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipokuja Arusha alikutana na farasi, mbwa na magari yaliyotanda kila kona alishangaa sana.
“Hawa polisi wanatumia nguvu kubwa kuwatawanya wapiga kura wangu, waliosimama barabarani kunipokea Mbunge wao, inasikitisha sana,” alisema.
Nassari alisema kuwa kamwe hatalia tena machozi yanayotokana na polisi wala kupeleka mashitaka kwao, sababu wana upendeleo wa chama kimoja.Katika hatua nyingine, Mbunge huyo amelishutumu Jeshi la Polisi wilayani Arumeru, kwa kuzuia mkutano wake wa hadhara akidai lina nia ya kumuhujumu kisiasa.
Alisema tangu aliposhambuliwa kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli Juni 16 mwaka huu, hajaweza kuonana na wapiga kura wake na kuzungumza nao kutokana na kulazwa hospitalini kufuatia kipigo alichopata.
“Nimekuwa nje ya jimbo kwa muda baada ya kushambuliwa huko Makuyuni Monduli, afya yangu imeimarika kiasi, hivyo, nikaona ni vyema nikarudi jimboni kwangu kuendelea na shughuli zangu za jimbo,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment