Askari polisi wa Wilaya ya Hai wakianda mwili wa mfanyabiashara wa madini Erasito Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Wasomali, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospiotali ya wilaya hiyo. Picha na Dionis Nyato
Moshi. Wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite katika miji ya Moshi, Arusha na Mirerani wamedai kutoshtushwa na mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa madini katika miji hiyo, Erasto Msuya.
Hata hivyo wamedai kilichowashtusha ni kuuawa kwa kumiminiwa risasi nyingi kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SMG hali inayotoa picha kwamba wauaji walikuwa na hasira iliyopitiliza.
“Sisi hatujashtushwa na kuuawa kwake kwa sababu hata kama wangempiga risasi mbili ama tano angekufa lakini kilichotustusha ni kuuawa kwa kupigwa risasi nyingi kiasi hicho,”alidai mmojawao.
Mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidokeza kuwa marehemu alikuwa amejijengea maadui wengi kutokana na biashara yake ya madini na shughuli nyingine.
Wafanyabiashara wengine waliohojiwa walidai kuna hofu imeanza kujengeka kwamba huenda kukajitokeza mauaji zaidi ya kulipiziana kisasi kati ya wafuasi wa marehemu na waliotekeleza mauaji.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment