KIKAO cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kilivunjika kwa mara ya pili baada ya Wabunge wa Tanzania, kutoka ndani ya ukumbi wakipinga kanuni kuvunjwa.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wenzetu, kudharau kiti cha Spika na kutaka kutoa hoja na kujadiliwa bila kufuata kanuni, sasa tumeona ni vizuri na sisi kwa kupinga kuvunjwa kanuni, tutoke ili kuonyesha tunapinga mchezo huu, haya yalikuwa ni maelezo ya mmoja wa wabunge wa Bunge hilo Abdullah Ali Hassan Mwinyi.
Mbunge wa Kenya, Peter Mathuki alitaka hoja yake ya kutaka utaratibu wa kufanyika kwa vikao vya bunge hilo kwa mzunguko ijadiliwe kitu ambacho kilipingwa na wabunge wa Tanzania, Hata hivyo Muthuki, juzi aliungwa mkono na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Tanzania.
Jana aliwasilisha hoja hiyo kwa kufuata utaratibu lakini haikujadiliwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje.
Katika hoja hiyo, msimamo wa wabunge wa Tanzania na Kamati ya Uongozi ya Bunge ni kuwa vikao vyote vifanyike katika ukumbi wa Bunge, Arusha baada ya Ukumbi huo kukamilika kujengwa.
ITV
3 comments:
Kama uwajui Wakenya na Kenyatta Jr wamuulinze Mchonga jinsi Kenya ya Kenyatta senior ilivyo tudhulumu mwaka 1977,walichukua almost kilakitu. Lazima tuwe makini kuanzia mwazo. Wanatabia ya kupima maji before they take action.
BINAFSI SIONI UMUHIMU WA JUMUIA. WE WILL BE BETTER OFF WITHOUT IT! KENYA ILISABABISHA KUVUNJWA KWA EAST AFRICAN COMMUNITY (EAC) IN THE 70s, SO WHY DO WE REPEAT THE SAME MISTAKES?
Mbona vikao vya viongozi wa AU(OAU)siku zote zinafayika Ethiopia.Au vikao vya UN ni New-York. Sasa kuanza kudai mzunguko huo ni ubinafsi .Any union which does not base on mutual relationship most of the time will not last. Mimi kama Mtanzania ni mashaka sana na hii EAC and I believe it will not last.We don't have to invest much on it. "We can do better without them," We have every thing swala hapa ni sisi wenyewe kujipanga,na sio kebembelezana na hao Manyang'au.Wasituletee za kileta,vikao viendelee kufanyika Arusha kama hawataki waka-----. Na huo uwe msimamo wetu hakuna kulegeza kamba.
Post a Comment