Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Holland..Rais Shein yupo nchini Holland kwa ziara ya kikazi.
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh: Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanzania wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein hapo jana katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag.
Mwenyekiti wa Tane nchini Uholanzi ndugu Kweba Bulemo akimkabidhi zawadi ya kitabu maalumu Mheshimiwa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kama kumbukumbu alipofanya mazungumzo na Watanzania hao hapo jana nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa ufafanuzi wa maswali yote aliyokuwa akiulizwa na baadhi ya Watanzania kuhusu mustakabari wa Kisiwani Zanzibar
Pichani ni mahudhurio ya watanzania waliojitokeza kuzungumza na Mh:Rais Ali Mohamed Shein hapo jana katika ukumbi wa hotel ya Hilton
Kati ya Watanzania waliouliza maswali ndugu Omary Abbas alikuwa mmoja wapo..pichani akiuliza moja kati ya maswali yake hapo jana.
Baadhi ya Watanzania wakiwa makini kabisa kusikiliza nini Rais anazungumza.
Wake kwa waume walijitokeza kwa wingi katika mkutano huo na Mheshimiwa Rais wakiwa makini kusikiliza
Maganga One Blogger akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hapo jana.
Maganga One Blogger akiwa na Mheshimiwa Balozi Diodorus Kamala hapo jana katika mkutano wa wa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi[Picha zote na maelezo toka http://magangaone.blogspot.com/ .. Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
1 comment:
Why tanzania bado ujinga upo...kama ni muungano why huyu jamaa anapewa presidential treatment kama yeye ni raisi wa tanzania. We should have one government kama kweli we are United republic of tanzania siyo what is right now. Nimeshajaribu elezea this unions in political studied and still the answer is wrong. We need one government period and save tax payer money wa zanzibar na tanganyika. ..
Post a Comment