Advertisements

Friday, September 27, 2013

MHE. MWIGULU NCHEMBA AFUNGUA TAWI LA CCM NORTH CAROLINA

Naibu Katibu wa CCM na Mbunge Mh. Mwigilu L. Nchema akikata tepe ya kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la CCM North Carolina. Kulia kwake ni Mlezi wa CCM North Carolina (aliyevaa nyekundu), akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi, Bwana David Mushi. Kushoto kwake dada Edna Ntirugelegwe (aliyevaa nyeusu) pia ni miongoni mwa kada wa siku nyingi wa CCM aliyewahi kushika nyadhfa mbalimbali za chama, akifuatiwa na dada Loveness.
 Juu na chini ni Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea na wanachama wapya wa CCM North Carolina mara tu alipomaliza kufungua tawi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM DMV Bi. Loveness Mamuya akiongea mawili matatu baada ya zoezi zima la ufunguzi wa tawi North Carolina kumalizika.

Tawi jipya la CCM North Carolina limefunguliwa rasmi September 26,2013 Durham North Carolina. Katika picha ya pamoja waliokaa kuanzia kushoto Katibu wa Tawi la CCM North Carolina Bwana Festo Mombo, wa pili yake ni Mh.Rajab Luhavi, wa tatu yake ni Mh. Mwigilu Lameck Nchemba na wa mwisho aliokaa ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM North Carolina (aliyevaa shati la kijani) ni Bw.David Mushi

Juu na chini ni Wanachama wa CCM NC wakifuatilia mkutano huku wangine wakiwa wameshikilia kadi zako.


makulaji yakiendelea.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.








1 comment:

Anonymous said...

Tumekimbia Bongo sababu ya CCM leo twaipenda?