Akanusha kukwamisha kesi kupinga sheria ya magazeti
Aelekeza lawama kwa mawakili wasiofika mahakamani
Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu
Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amesema Mahakama Kuu isilaume kwa kuchelewa kusikilizwa kwa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kampuni ya Halihalisi Publisher Ltd ya kupinga sheria ya magazeti ya mwaka 1976 dhidi ya Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, kwani mawakili ndiyo wamekuwa hawafiki mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
Alitoa kauli hiyo ilitolewa wakati wa mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu tuhuma zinazotolewa kwamba kesi hiyo haijawahi kupangiwa jopo la majaji wa kuisikiliza.
Alisema amesikitishwa sana na baadhi ya watu wanavyoiongelea Mahakama bila kuwa na uthibitisho kwamba kesi hiyo haijawahi kupangiwa jopo la majaji tangu mwaka 2009.
Alisema kesi hiyo namba 34 ya mwaka 2009 ilipangiwa jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Projest Rugazia, Radhia Sheikh na Crecensia Makuru.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama, jalada la kesi hiyo linaonyesha kwamba jopo hilo liliketi kwa mara ya kwanza Desemba 3, mwaka 2009 Kampuni ya Halihalisi inayochaopisha gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa mwaka jana kwa muda usiojulikana, iliwakilishwa na Wakili Mwandamizi Gabriel Mnyelle na walalamikiwa waliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata.
Hata hivyo, mawakili wa pande zote mbili walipewa muda kwa ajili ya kujibishana nyaraka za kisheria.
Aidha, kesi hiyo iliendelea kutajwa na kuahirishwa mara kwa mara mahakamani hapo kutokana na mawakili wa pande zote mbili kutokuwapo ama wakati mwingine walihudhuria wa upande mmoja tu.
“Jopo lilipanguliwa baada ya Jaji Maruku kuhamishiwa Moshi, Jaji mfawidhi alilipanga shauri hilo kwa Jaji Augustino Mwarija tangu mwaka 2012, lakini mawakili hawafiki kusikiliza kesi yao sasa itasikilizwaje?” alihoji Jaji Kiongozi.
Akifafanua zaidi, Jaji Kiongozi alisema: “Wanaolalamika huko mitaani bila kuwa na uhakika na kile wanachokisema wanakosea, waje hapa mahakamani wapate ufafanuzi na ukweli uko vipi.”
NIPASHE ilipata nafasi ya kuangalia kumbukumbu hizo za mahakama ambazo zinaonyesha kuwa tangu Oktoba 27, mwaka 2012 jalada lilikuwa mbele ya jopo hilo, lakini mawakili wote hawakuwapo mahakamani.
Kesi hiyo iliahirishwa tena Septemba 13, mwaka huu na Msajili Amir Msumi kutokana na mawakili kutokuwapo.
Kesi hiyo kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama, imepangwa kusikilizwa Februari 10, mwaka 2014.
Jaji Jundu alisema kuwa Mahakama haina sababu za kutoisikiliza kesi hiyo, bali kikwazo kikubwa ni mawakili wenyewe.
Kampuni hiyo inapinga kifungu cha 3 cha sheria hiyo ambacho kinatoa mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari kufunga gazeti wakati wowote bila gazeti husika kupewa fursa ya kutoa utetezi au kukata rufani.
Sheria hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu kwamba imepitwa na wakati na inabana uhuru wa habari nchini.
Sheria hiyo pia ilitumiwa na serikali Septemba 27, mwaka huu kuyafungia magazeti ya MWANANCHI kwa siku 14 na Mtanzania siku 90 kwa madai ya kuandika habari za uchochezi kwa lengo la kuwashawishi wananchi kutokuwa na imani na vyombo vya dola.
Sheria ya Magazeti namba tatu ya mwaka 1976 ni miongoni mwa sheria 40 ambazo Tume ya Jaji Francis Nyalali aliyeongoza Tume ya kukusanya maoni ya vyama vingi mwaka 1992, kutangaza kuwa ni kandamizi na inapaswa kufutwa au kurekebishwa ili iendane na mazingira ya mfumo wa vyama vingi nchini.
Miaka 20 na ushei sasa bado serikali imeendelea kung’ang’ania sheria hiyo na katika mkutano wa bunge unaokuja imewaandaa marekebisho ya sheria hiyo kwa nia ya kuongea adhabu kwa waandishi wa habari juu ya kifungo na faini.
Katika muswada wa marekebisho ya sheria mballimbali serikali inataka sheria ya magazeti iongezewe makali kwa kuwapiga faini ya Sh. milioni tano waandishi kutoka za zamani ya Sh. 150,000.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment