ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 15, 2013

KESI YA BABU SEYA KUANZA KUSIKILIZWA UPYA TAREHE 30 MWEZI HUU!!


Papi Kocha aka Mtoto wa mfalme akiwa na baba yake Mzee Nguza aka Babu Seya 

MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe. Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo. 

Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.
Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha’, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.

3 comments:

Anonymous said...

Default Re: Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30
wakiwa court of Appeal wakili mabere marando alisikika akisema "katika umri wangu wote sijawahi sikia ama kuona mtoto wa miaka chini ya nane akaingiliwa na mtu mzima kisha mzazi wake asigundue siku ileile hadi mtoto alipoanza kuoza "

hebu tufikiri kwa pamoja, watoto zaidi ya watano walikua below eight wakati huohuo wanadai waliingiliwa mara kadhaa na watoto wa babu seya na babu seya mwenyewe, well ! sasa tuamini kuwa wazazi wa watoto wale wote walikuwa si waangalifu kuweza kutambua hilo mapema ? kwa watoto wetu hawa mpaka darasa la tatu wanaogeshwa na kufuliwa nguo hadi za ndani !>? tujiulize damu hazikuwatoka ? je madoa hayakubaki kwenye chupi zao >? ingekuwa mmoja unaweza kusema kiwango chake cha uvumilivu labda ni kikubwa, lakini kwa watoto zaidi ya watan ? hapana...maana mtu mzima mwenyewe akiingiliwa bila ridhaa cha moto anakiona sembuse hao watoto wadogo hivyo >?

nami naungana na wengine kuona mashaka makubwa ya ushiriki wa familia nzima kuwanajisi watoto wadogo hao .

Anonymous said...

kama vipi wahasiwe wasifanye tena tendo hili wakongo ndo zao tena wanafanya haya kwa ushirikina wao usisikiye aiseeee yesuu yangu na maria

Anonymous said...

Jamani Ndugu Watanzania wenzangu. Mambo mengine ni lazima tujiulize mara mbilimbili. Siyo rahisi Baba mtu mzima pamoja na Watoto wakaamua Kuwaingilia watoto wadogo hao. Ingekuwa ni kweli si wangewaingilia Madada/Wamama? Binadamu tujifunze Kusamehe ili nasi Tuweze Kusamehewa na Mwenyezi Mungu wetu. Mungu pekee ndiye atakaetuhukumu. Mahakumu siku hiyo ikifika Wasameheni Wanaume wenzenu. Inawezekana Walisingiziwa tuu!! Kama kweli hawakutenda Tendo hilo Mungu mwenye Wingi wa Rehema ukawanyoshee Mkono wako na Kuwawezesha ili Serikali na hasa Rais wetu Mheshimiwa J.K. ili nawewe uje Usamehewe Dhambi zako. Mimi simjui Babu Seya wala Mtoto wake, bali ni Mwanadamu tu. Hakuna aliyekamika, wote tunahitaji Kusamehewa. Amen.